Wananchi wa
kata ya lwangwa Halmashauri
ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameandamana
kuanzia leo asubuhi
hadi katika ofisi za Halmashauri hiyo
wakishiniza serikali wilayani
humo kuwatoa watu
walio kamatwa baada ya kuhusiwa kuhusika na kifo cha
Gabriel Mwandemwa mwenye umri wa mika
{40} aliye uwawa na wananchi
katika siku za hivi karibuni kutokana na imani za kishirikina.
Wakizungumza
na yetu rungwe blog wakati
wa mandamano hayo wanachi
hao walisema hatua hiyo ilikuja
kufuatia jeshi la polisi wilayani humo
kuwakamata baadhi ya wananchi kwa madai ya
kuhusika na kifo cha kijana huyo
aliyefariki dunia siku za hivi karibuni
kutokana na vitendo vya
ushirikina.
Walisema
mnamo majila ya usiku wa kuamkia oktoba
moja jeshi la polisi liliwasili kinyemela katika maeneo hayo
kwa kuwakamata baadhi ya
wananchi bila kushirisha uongozi wa
maeneo husika kwa kufikishwa
kituoni, ambapo kutokana na
hali hiyo iliweza kupelekea wao kama
wanachi kuchukua hatua ya
kupinga kitendo hicho kwa
kuungana kwa pamoja
na kufanya maadamano ya amani
hadi katika ofisi ya mkurugezi
wa Halmashauri hiyo wakitaka
kutolewa kwa ndugu zao.
Hata
hivyo jeshi la polisi
liliwasili eneo la
tukio na kisha kunza kusaidia kuzuia gasia
hizo ikiwa ni pamoja
na kuwatia hatiani wale wote ambao walionekana kuanzisha vurugu hizo.
Diwani wa kata hiyo Robati Mwaibata alikili kuwapo kwa adha hiyo
na kusema mpaka sasa
wameshindwa kuongea na wananchi wake kutokana na
vurugu kuendelea kuchukua nafasi
yake.
Alisema chanzo
cha tukio hilo ni
baada ya jeshi la polisi kuwakamata
baadhi ya vijana wa eneo hilo
kwa tuhuma za
kuhusika na mauji
ya Gabriel Mwandemwa aliye
fariki dunia siku za hivi karibuni
kwa kukatwa na mapanga na kisha mwili wake kuchomwa moto.
Alisema mpaka sasa wanaendelea kutuliza gasia hizo kwa
ushirikiana na jeshi la polisi wilayani humo .
Hata
hivyo juhudi na malfa za
kutafuta mkuu wa wilaya ya rungwe krspini meela ziligonga mwamba mara
baada ya simu yake
kuita bila kupokelewa.
Siku
za hivi karibuni
wananchi wa kijiji cha Ikama
Mbande walimkamata Gabliel
Mwaibata walimkamata kwa kumwachia
kipigo na kisha kumchoma moto
baada ya kudaiwa kujihusisha
na vitendo vya kishjirikina.