MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) APIGWA DANA DANA KUHUSIANA NA UHAMISHO YADAIWA PICHA ZAKE ZIMEPOTEA
Amina akiangua kilio mbele ya afisa elimu msaidizi kutokana na kutojua hatima yake na maisha yake ya baadae
Amina akijieleza jinsi alivyodharilishwa na kunyanyaswa hadi kupelekea kulala kwa mlinzi kutokana na vitisho vya wanafunzi wenzake
Amina akiwa ofisini kwa mkuu wa shule akifuatilia uhamisho wake
Baadhi ya wanafunzi wakiwa nje ya jengo la utawala wakisubiri kutoa maelezo kwa mwandishi
Hata hivyo cha kushangaza mwandishi wetu alikuta bendera ya Taifa ikishushwa saa moja jioni hali wengine wakiendelea na shughuli zao hapo shuleni kitu abacho ni kinyume na masharti ya ushushwaji wa bendela hiyo
Siku chache mara baada ya Mwanafunzi wa kidato cha tatu kwa katika shule ya secondari Hollywood iliyopo wilayani momba mkoani mbeya Ndugu Amina Mwamkinga (20) kutimuliwa shule takribani Miezi Miwili kwa madai kuwa anajihusisha na imani za Kishirikina ameendelea kusota mtaani huku akishindwa kujua nini hatma ya maish yake ..
Mara baada ya kupokea kwa taarifa hiyo Afisa Elimu Wilaya ya Momba Ndugu Izack Mgaya alilazimika kumuita Mkuu wa shule hiyo kwa lengo la kupata maelezo ya kina juu ya kuwepo kwa sakata hilo la mwanafunzi kufukuzwa shule .
Mkuu huyo wa shule hiyo Ndugu Imani Mtafya ambaye mara baada ya kuitwa na afisa elimu huyo alikili kutokea kwa sakata hilo la mwanafunzi ambapo alieleza kuwa licha ya mwanafunzi kutuhumiwa kwa ushirikina hakupatiwa nafasi ya kujieleza juu ya yeye kutuhumiwa kwake na vitendo vya ushirikina na uongozi wa shule hiyo.
Baada ya maelezo hayo kutoka kwa pande zote mbili afisa Elimu aliagiza mwanafunzi huyo kupatiwa uhamisho kwenda shule nyingine ili aendelee na masomo yake licha ya mwanafunzi huyo kusimama kuendelea na masomo yake kwa kipindi cha miezi mitatu sasa.
Hata hivyo baada ya mwanafunzi huyo kufika shuleni hapo kwa lengo la kupata uhamisho huo alielezwa na uongozi wa shule hiyo ya Hollywood kwamba picha zake pamoja na taarifa nyingine zimepotea hivyo kufanya mwanafunzi huyo kutapatapa na kutofahamu nini cha kufanya.
Kufuatia hali Amina Mwamkinga ambaye ni mlemevu wa ngozi (Albino) ameziomba asasi mbalimbali pamoja na serikali kumsaidia ili kufahamu hatima ya maisha yake ya baadaye pamoja na kutoa wito kwa jamii kutambua kuwa watu wenye ulemavu wa ngozi wanahaki ya kupata elimu kwa watu wengine hivyo wasiwatenge .
Machi 9, Mwaka huu wanafunzi wa shule hiyo walimtuhumu binti huyo kujihusisha na vitendo vya kishirikina ambapo uongozi wa shule hiyo uliamua kumtimua mwanafunzi huyo bila kupata maelezo ya kina.
Mhanga wa tukio hilo Amina Mwankinga amesema tangu kipindi hicho alipofukuzwa bwenini na wanafunzi wenzie wakitaka aondoke shuleni hapo majira ya usiku hali iliyomlazimu kuomba hifadhi kwa mlinzi aliyemkubalia na kukesha naye hadi asubuhi hali iliyopelekea kupigwa na baridi kali kutokana na kukosa nguo za kujisitiri kama Shuka nk.
Amesema kutokana na hali hiyo Walimu pamoja na uongozi wa Shule hiyo haukuchukua hatua yoyote jambo lililomlazimu kuondoka Shuleni hapo baada ya kukosa msaada ambapo alirejea Jijini Mbeya anakoishi na Binamu yake.
Binti huyo anayesomeshwa na Shirika la Under the SameSun iliyoko Jijini Dar Es Salaam ameomba msaada kwa wasamaria wema kumtafutia Shule ili aendelee na masomo kwa ajili ya kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne Mwakani.
.
Naye katibu wa Chama cha Albino Mkoa wa Mbeya, Wiliamu Simwale amesema alikuwa halijui suala hilo na kwamba kama lingekuwa suala liko nyeti angejulishwa yeye juu ya hatua zilizofikiwa ambapo Uongozi wa Shule umeendelea kupokea fedha za malipo ya Mwanafunzi pasipo kutoa taarifa kwenye shirika linalolipa.
Awali Mlezi wa Wanafunzi hao kutoka Shirika la Under the Samesun Omary Mfaume amesema kwamba hana taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo na kuongeza kuwa anawasiliana na uongozi wa Shule moja kwa moja ili umweleze juu ya kilichotokea ili taratibu za kumtafutia Shule nyingine zifanyika haraka ili Mwanafunzi aendelee na masomo kama kawaida.
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) APIGWA DANA DANA KUHUSIANA NA UHAMISHO YADAIWA PICHA ZAKE ZIMEPOTEA
ReplyDeleteAmina akiangua kilio mbele ya afisa elimu msaidizi kutokana na kutojua hatima yake na maisha yake ya baadae