Thursday, November 6, 2014

JAMAA ADAIWA KURUBUNI WAKE ZA WATU KINGONO ANASWA

Wakinamama (kushoto) wakimficha mwenzao (mke wa mtu) aliyenaswa kwenye ghetto la njemba mwenye asili ya Kiarabu, Hemed.

Mji wa Morogoro umekumbwa na matukio mfululizo ya mafumanizi ambapo baada ya ticha wa shule ya msingi kufumaniwa na dereva wa bodaboda kisha jamaa kubondwa kwa kukutwa akifanya ngono na mke wa mtu vichakani na denti wa upadri kufumaniwa, mwanzoni mwa wiki hii fumanizi lingine kiboko la njemba mwenye asili ya Kiarabu limetokea.Kwenye Kata ya Mazimbu mjini hapa mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Hemed, anadaiwa kunaswa laivu na mke wa mtu kwenye chumba anachoishi kilichopo Mtaa wa Boma mjini hapa.
Ikiwa kazini, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilinyetishiwa kuwepo kwa ishu hiyo hivyo kufika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri na kunasa tukio hilo likiwa bichi.
Wakinamama hao wakifanya juhudi kumtoa mke wa mtu (mwenye sidiria) eneo la tukio.
Katika fumanizi hilo lililojaza ‘inzi’ (umati), Hemed alidaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwarubuni na kumwaga fedha mbuzi kwa wake za watu na kuserebuka nao ndani ya ‘geto’ lake jambo lililowafanya wenye wake zao kumwekea mtego ambao ulipofyatuka ukamnasa majira ya saa 3:00 asubuhi.
Akihojiwa na gazeti hili, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema kuwa, jamaa huyo alikuwa na mwanamke mzuri wa umbo aliyetajwa kwa jina moja la Husna ambaye alikutwa chumbani kwa Hemed.
Mashuhuda wa tukio hilo wakipiga chabo dirishani kwa mwarabu aliyenaswa.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwenye eneo la tukio, mume wa Husna aliyejitambulisha kwa jina moja la Siri alikuwa na haya ya kusema:
“Nilimuaga mke wangu nakwenda Mwanza kwenye shughuli zangu za biashara. Nikiwa Mwanza nilijulishwa na majirani kwamba mke wangu kila siku anaacha watoto wetu kwa mama yake na kwenda kulala kwa Mwarabu.
Raia wenye Hasira kali wakiwa eneo la tukio.
“Ukweli kama mwanaume nilipatwa na hasira, nikatafuta ndege nikarudi hapa (Morogoro).
“Nimeelekezwa kwa Mwarabu na jamaa waliokuwa wamemwekea mtego, nilipofika nilichungulia dirishani, nikamuona mke wangu na Mwarabu wakiwa kitandani.
“Nilihisi kupooza mwili na roho ilikuwa inaniuma sana.”
Mwarabu(mwenye koti jekundu) aliyenaswa na mke wa mtu akiwa chini ya ulinzi.
Aliongeza: “Mimi na mke wangu tumefunga ndoa ya Kiislamu, tuna watoto wawili, mmoja ana umri wa miaka mitano na wa pili ana mwaka mmoja na miezi saba.
“Cha ajabu mtoto wa pili hadi sasa hatembei. Kwa tukio kama hili nahisi mke wangu amembembenda.”
Mtuhumiwa (mwarabu) akichukuliwa kwa mahojiano zaidi.
Kwa upande wake Husna ambaye alisitiriwa na wanawake wenzake waliokuwa wakimficha, alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo, alimjia juu mwanahabari wetu na kumtolea maneno ya shombo. 
Naye Mwarabu huyo alipohojiwa, pia alimtolea vitisho ‘kamanda’ wetu.
Kufuatia wingi wa watu, wawili hao walifungiwa chumbani lakini raia wenye hasira kali wakavunja mlango na kuwashushia kichapo.
Baadaye viongozi wa Kata ya Mazimbu wakiongozwa na Afisa Mtendaji, Brioht Sospeter na polisi mmoja walifika eneo la tukio wakawaondoa wawili hao na kuwapeleka ofisi ya kata kwa mahojiano zaidi.

BASI LAGONGA TRENI NA KUUA WATU 12

Basi la Super Aljabir baada ya ajali.
watu 12 wamepoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa baada ya Basi la Super Aljabir linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Mahenge mkoani Morogoro kugongana na treni maeneo ya Kiberege karibu na Ifakara, Morogoro jioni hii.Ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likijaribu kuwahi kuvuka reli kabla ya treni kupita.
Baadhi ya miili katika ajali hiyo ikiwa eneo la tukio.

AKAMATWA AKIWA ANASAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA KWA ‘’STYLE’’


unnamedPichani mtuhumiwa Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa aliyekamatwa eneo la Mianzini jijini Arusha akiwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi iliyokuwa inasafirishwa toka nchi jirani ya Kenya kuelekea Kondoa mkoani Dodoma (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Mtu mmoja aitwaye Hamis Mohamed (47) Mkazi wa Kondoa mkoa wa Dodoma, amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha baada ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi aliyekuwa anaisafirisha kwa mtindo wa aina yake.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas alisema kwamba tukio hilo lilitokea tarehe 05.11.2014 muda wa saa 11:00 jioni eneo la Mianzini ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa anasafirisha madawa hayo kwenye gari aina ya Fusso basi lenye namba za usajili T. 577 BFM ambapo aliihifadhi kwenye magunia mawili huku juu na pembeni ya magunia hayo akiweka viatu.
‘’Katika magunia yale alikuwa ameweka viatu na katikati aliweka viroba 36 vya madawa hayo aina ya mirungi ambayo alikuwa anasafirisha toka nchini Kenya kupeleka Kondoa mkoani Dodoma hivyo ukiangalia unaweza kusema ni viatu pekee’’. Alifafanua Kamanda Sabas.
Alisema tukio hilo lilifanikiwa kutokana na mahusiano mema yaliyopo kati ya Jeshi hilo na raia wema ambao walitoa taarifa iliyofanyiwa kazi haraka na asakari wa Jeshi hilo.
Baada ya askari hao kupata taarifa hiyo walianza kulifuatilia gari hilo na lilipofika maeneo ya Mianzini jijini hapa kwenye maegesho ya basi hilo ndipo walipoanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kukamata magunia hayo yaliyokuwa na viatu vilivyochanganywa na madawa hayo.
Kamanda Sabas alisema kwamba mtuhumiwa huyo bado anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

IGP AFANYA MABADILIKO NDANI YA JESHI LA POLISI



Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora.

Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala. Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
Imetolewa na: 
Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi

GADNER AMPANDISHA KIZIMBANI LADY JAYDEE


Mke wa Gardner G Habash, Judith Wambura Mbibo, ‘Lady Jaydee’ akipozi.
Prizenta aliyetua Radio E-FM hivi karibuni akitokea Radio Times FM, Gardner G Habash ‘Kapteini’ anadaiwa kumpandisha kortini mkewe, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ kisa kikisemekana ni mgawanyo wa mali hivyo anataka haki yake baada ya kuwepo kwa madai mazito ya ndoa yao kuvunjika.Kwa mujibu wa madai hayo, inasemekana kwamba Gardner amekimbilia mahakamani akidai apewe talaka na waweze kugawana mali walizochuma wote ili kila mmoja achukue hamsini zake.
Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa familia hiyo kililiambia gazeti hili kwamba, siku chache baada ya kutengana na huku hali ikizidi kuwa mbaya, mtangazaji huyo alichukua hatua ya kutafuta msaada kwa wanasheria.
“Msinitaje jina ila ninachowaambia ni kwamba Gardner tayari ameshampata mwanasheria anataka kumshitaki Jaydee.
“Anachohitaji ni kugawana mali zao, kila mtu afanye maisha yake na ukiangalia tu Gardner hana mpango tena wa kuendelea na maisha ya ndoa na Jaydee ila Jide yeye bado ana matumaini ya kurudiana wawe pamoja na hasa kinachomuuma ni kugawana mali.
 
Prizenta wa Radio E-FM hivi karibuni Gardner G Habash ‘Kapteini’ Lady Jaydee
“Yaani Gardner ameshafanya kila aina ya jitihada ya kutaka waachane kiroho safi lakini Jaydee anaonekana kutokubaliana na wazo hilo kwani anaogopa ule usemi kwamba mwanamke mjinga huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:“Ishu ya kugawana mali ya Gardner na Jide ndiyo habari ya mjini na ili jamaa apate chake ameona heri atafute mkono wa sheria.”
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, kitendo cha Jaydee kutangaza kubadili mwelekeo wa mali zake akianza kwa kubadili jina la ule mgahawa wake kutoka lile la Nyumbani Lounge na kuuita M.O.G ndicho kimemshtua Gardner na watu wake wa karibu.
Kilendelea kudai kwamba, pia ishu ya Jaydee kubadili jina la Bendi ya Machozi na kuiita Lady Jaydee and the Band, nayo imemchochea Gardner na kuamua kukimbilia mahakamani. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Gardner ili aweke wazi madai ya kutaka kumburuza mahakamani mkewe huyo na haya ndiyo majibu yake mafupi: “Kaka kusema kweli hiyo ishu nashindwa kuizungumzia maana hata sijui wewe umeipata wapi dah.”
Gardner na Jaydee ambao walifunga ndoa mwaka 2005, wamekuwa wakidaiwa kuwa hawapo pamoja tena huku majukumu ya mtangazaji huyo ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki huyo yakichukuliwa na ndugu wa Jide ambaye ni Wakazi

MATOKEO YA WAHITIMU DARASA LA SABA 2014



MZEE WA UPAKO AMIMINA RISASI MTAANI!

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ akitafakari jambo. Ishu hiyo iliyojaa utata mkubwa, ilitokea saa nne usiku maeneo ya Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam kwenye barabara inayotoka barabara kuu kwenda kanisani kwake. 
NI kama kimenuka tu! Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ usiku wa kuamkia Jumatatu iliyopita alizua la kuzua kufuatia kumimina risasi kadhaa hadharani kwa madai ya kuwatawanya kundi la vijana waliodaiwa kumvamia na kuziba barabara kwa lengo la kumfanyia kitu mbaya.
 
MAELEZO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, tukio lilianza kwa Mzee wa Upako aliyekuwa akipita kwa miguu kukejeliwa na vijana waliomwita Freemason kauli ambayo mtumishi huyo wa Mungu aliiona ni ya kejeli kwake.“Baada ya kuitwa Freemason, yule kijana akiwa na wenzake waliendelea kumkejeli Mzee wa Upako, akawafuata na kuwauliza mbona mnanitukana, nimewakosea nini?” 
RISASI ZARINDIMA
“Alipoona wale vijana wanazidi kumkejeli huku wakionesha dalili za kumfanyia fujo ndipo alipotoa bastola yake na kufyatua risasi tatu juu hali iliyowafanya wale vijana kutawanyika huku na kule.
“Baadhi ya watu walikuwa kwenye biashara zao, nao walitimua mbio, wengine waliacha biashara, unajua risasi ni risasi tu, mtu akisikia risasi hawezi kukaa salama hata kama ni mjeshi,” kilisema chanzo hicho.
Moja wapo ya alama zinazoaminiwa kuwa ni za Freemasons MZEE WA UPAKO ATIMUA MBIO
Ilizidi kudaiwa kwamba, kufuatia kimbiakimbia hiyo, Mzee wa Upako naye alikimbia. Baadaye alirudi eneo la tukio kimachale na kukuta watu wameanza kukusanyika kujua kulikoni.“Mzee wa Upako alipofika aliagiza mtu atakayeokota ‘magazini’ ya risasi alizofyatua angempa shilingi alfu ishirini, vijana wengine wakaingia kazini, wakapata moja, wakapewa chao, Mzee wa Upako akasema mtu akiokota nyingine aipeleke polisi,” kilisema chanzo. 
MADAI YA WATU
Kuna madai kwamba, vurugu hizo zilipambwa na kijana mmoja anayeitwa Robert ambapo mtumishi huyo wa Mungu alimkomalia kuwa ndiye aliyekuwa akiongoza wenzake kumtukana na kumkashifu kwamba yeye ni Freemason na si mchungaji wa kiroho kama anavyojiita. 
MZEE WA UPAKO NA GAZETI LA AMANI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili lilimtafuta Mzee wa Upako kwa njia ya simu na alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea na kueleza ‘full’ mkanda.“Ni kweli lilitokea. Ni kwamba, siku hiyo nilipofika eneo lile kuna vijana wa kihuni walinifuata kwa nyuma, wakaanza kupigapiga gari langu, wengine wakizuia njiahuku wakidai eti mimi ni Freemason.
Mfano wa silaha ya moto (bastola) kama ile ya Mzee wa Upako. “Nilijaribu kuwaambia kwamba mimi ni kiongozi wa kiroho lakini badala yake wakaanza kuniangushia matusi. Ili kujiokoa nilifyatua risasi hewani kuwatawanya,” alisema Mzee wa Upako.Alipoulizwa kama anaweza kujua sababu za watu hao kumvamia na kumwambia yeye ni Freemason, kiongozi huyo alisema:
“Siwezi kujua, lakini mara baada ya kufyatua risasi na wao kutawanyika mimi niliamua mwenyewe kwenda Kituo cha Polisi Urafiki (Dar) kutoa taarifa.“Mimi siwezi kujua sababu za watu hao kunikashifu na kunitukana labda ukiwapata watakuambia lakini ni watu ambao naamini wametumwa na mtu f’lani ambaye mimi siwezi kukwambia lakini polisi watamjua baada ya upelelezi wao,” alisema. 
Alipoulizwa alikuwa anatoka wapi usiku huo, Mzee wa Upako akajibu kwamba alikuwa anawenda kanisani kwake Ubungo Kibangu kwenye shughuli zake za kawaida za kiroho. 
MADAI YA ROBERT
Madai ya upande wa Robert anayedaiwa kuongoza vijana wenzake kumfanyia vurugu Mzee wa Upako yanasema kuwa, baada ya mtiti huo wa risasi, yeye alikimbilia Kituo cha Polisi Mbezi, Dar na kufungua malalamiko yenye Kumbukumbu Na. JMD/RB/11099/2014 KUTISHIA KUUA KWA RISASI!Hata hivyo, Robert alipopigiwa simu ili kuulizwa kwa undani hakupokea licha ya kuita kwa muda mrefu na kutumiwa meseji kwa namba yake ya simu.