Sunday, August 24, 2014
AMEFUNGUKA MWENYEWE
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka
hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es
Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia
hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie
harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu
kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu
ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani
waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa
sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta
umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya
Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema:
“Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili
wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda
mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana
vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na
kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali
huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema:
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi
yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha
baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake
huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini
hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.
“Lakini ninachoweza kukwambia ni kuwa sisi ndio tunaoujua ukweli wa uhusiano wetu.
“Sidhani kama ni sahihi mapenzi yetu yakawa na wasemaji wengine zaidi yetu wenyewe. Sasa ni ajabu watu wanaposema yao.”
Credit: Mwanaspoti
Credit: Mwanaspoti
PINDA AFUNGUA HARAMBEE YA MKAPA FELLOWS
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika harambee ya kuchangia Mradi wa
Mkapa Fellows kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014.
Zaidi ya sh. Bilioni 1.3 zilichangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mchango wa shilingi milioni 15 kutoka kwa
Mfanyabiashara wa Mwanza na Dar es salaam Jumanne Kishimba katika
harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyiak kwenye hoteli
ya JB Belmont jijini Mwanza August 23,2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni
1.3 zilichangwa. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimshukuru Mfanyabiashara wa
Dar es salaam na Mwanza, Jumanne Kishimba ambaye alichangia Shilingi
milioni 15 katika harambee ya kuchangia mradi wa Mkapa Felllows kwenye
hotel ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi
Bilioni 1.5 zilichangwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkapa HIV/AIDS,
Balozi Charles Sanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mmuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal
Fabian Massawe Maarufu kwa jina la Mulokozi mchango wa zaidi ya shilingi
milioni 100 zilizochangwa na Wanakagera katika harambee ya kuchangisha
fedha kwa ajili ya Mradi wa Mkapa Fellows, kwenye hoteli ya JB Belmont
jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni1.3 zilichangwa
katika harambee hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Mizengo Pinda akipokea mchango wa zaidi ya shilingi milioni 100
kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Ali Rufunga zilizotolewa na
wanashinyanga kuchangia mradi wa Mkapa Fellows katika harambee
iliyoongozwa na Waziri Mkuu kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza
August 23, 2014. Zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi
Evarest Ndikilo ambaye aliwasilisha mchango wa zaidi ya Shilingi
milioni 100 zilizochangwa na Wanamwanza katika harambee ya kuchangia
Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont jijini
Mwanza, August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa
katika harambee hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
RAIS KIKWETE AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI MJINI MOROGORO,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
(MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na
Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wataalamu walioshughulikia ufungwaji wa mtambo huowakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Morogoro mjini Mhe Aziz Aboud wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa wadau wa mji wa Morogoro wakati akiwasili eneo la Mambogo katika manispaa ya wilaya ya Morogoro tayari kukagua na kufungua rasmi mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Jengo la mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Baadhi ya wafanyakazi wa MORUWASA wakishangilia wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mradi mkubwa wa maji ambao umegharimiwa na Serikali ya Marekani kupitia MCA-Tanzania Agosti 22, 2014
Burudani wakati wa sherehe hizo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Joel Bendera akifungua pazia la sherehe hizo
Sehemu ya jengo la mradi huo
Kwa ubavuni
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu akitoa muhtasari wa mradi huo
Bango linajieleza
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakati wa sherehe hizo
Rais Kikwete akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MCA-Tanzania Mhe Bernard Mchomvu kwa kufanuikisha mradi
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiongea machache
Mama Salma Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika
la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher
akisoma hotuba yake kwa Kiswahili wakati wa sherehe hizo
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhe Mbogo Futakamba akiongea wakati wa
sherehe hizo na kumkaribisha Rais Kikwete aongee na wananchi
Rais Kikwete akizungumza na kuzindua rasmi mradi huo mkubwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifunua pazia kuzindua mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakifurahgia baada ya kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akibofya kitufe kupiga king’ora kuzindua rasmi mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikata utepe kuzindua mradi huo
Rais Kikwete akipata maelezo ya mradi toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASA
Sehemu ya mitambo ya mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-Tanzania) Bw. Karl Fickenscher wakikagua mitambo ya mradi huo
Mkurugenzi Mkuu wa MORUWASCO Bw. Nicholaus Angumbwike akiendelea kutoa maelezo ya mradi
Ukaguzi ukiendelea
Ukaguzi wa sehemu ya kusafishia maji
Subscribe to:
Posts (Atom)