Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman (hayupo pichani).…
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe
Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba
16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns
Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka
katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania
Mhe Ibrahim Juma ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini
Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani
Mhe Liberata Mulamula aliyesindikiza msafara wa Jaji Mkuu wa Tanzania
Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014 Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania
Mhe Ignass Kitusi ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe
Hussein Katanga. ambaye ni mmoja wa wajumbe wa msafara wa Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman walipokwenda kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Meja Jenerali Adolph Mutta ambaye
alimsindikiza Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda
kumjulia hali jijini Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014. Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani Dkt. Sweetbert Mkama ambaye alimsindikiza Jaji Mkuu wa
Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman kwenda kumjulia hali jijini
Baltimore, Maryland, Jumapili Novemba 16, 2014.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Siha ,Rashid Kitambulilo akimuongoza mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea eneo la
mwekezaji la Tanganyika Film and Safari ambako wafugaji jamii ya Masai
wanadaiwa kufanya uharibifu mkubwa.…
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Siha ,Rashid Kitambulilo akimuongoza mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea eneo la
mwekezaji la Tanganyika Film and Safari ambako wafugaji jamii ya Masai
wanadaiwa kufanya uharibifu mkubwa.Mkuu
wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na kamati ya ulinzi na
usalama wakitizama uharibifu uliofanywa na wafugaji jamii ya Masai.Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitizama moja ya gari
lililochomwa moto na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji jamii ya Masai.Mkuu wa mkoa ,Gama akiteta jambo na baadhi ya viongozi ambao ni wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama.Vikao vikiendelea eneo la mwekezaji.
Uharibifu mkubwa umefanyika ambapo nyumba 16 na magari tisa yameteketea moto.Mwekezaji Peter Jones akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo lililomsababishia hasara kubwa.
Vikosi vya askari Polisi
kutoka Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro vililazimika kupiga kambi kwa muda
katika eneo hilo ili kuwadhibiti wafugaji hao.Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii kanda ya kaskazini.
RIPOTI ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG),
kuhusu kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 200, kwenye Akaunti
ya Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
umeanika madudu mazito yaliyofanywa na vigogo wa Serikali, Tanzania
Daima limedokezwa. Ingawa ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima limebahatika kuiona,
imekwepa kutaja majina ya vigogo hao na taasisi wanazotoka, lakini
inaonyesha kuwa jumla ya fedha za Escrow ni sh bilioni 306 ambazo ni
matokeo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kulipishwa tozo la
uwekezaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa. CAG katika ripoti hiyo,… RIPOTI
ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), kuhusu
kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 200, kwenye Akaunti ya
Tegeta Escrow zilizohifadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
umeanika madudu mazito yaliyofanywa na vigogo wa Serikali, Tanzania
Daima limedokezwa. Ingawa ripoti hiyo ambayo Tanzania Daima limebahatika kuiona,
imekwepa kutaja majina ya vigogo hao na taasisi wanazotoka, lakini
inaonyesha kuwa jumla ya fedha za Escrow ni sh bilioni 306 ambazo ni
matokeo ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kulipishwa tozo la
uwekezaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa. CAG
katika ripoti hiyo, anasema Tanesco walipaswa kurejeshewa sh bilioni
321 zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002 – 2012. “Hivyo fedha za Escrow ni fedha za umma, yote ilipaswa kurudi Tanesco
na shirika kuendelea kuwadai IPTL sh bilioni 15,” alisema CAG. Madudu mengine yaliyoibuliwa katika ripoti hiyo ni kwamba, kampuni ya
PAP haikununua kihalali hisa 70% za kampuni ya Mechmar katika IPTL
kwani zilizuiwa na Mahakama, hivyo hawana hati halisi za hisa na PAP
ilifanya udanganyifu katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uwongo
na kuikosesha Serikali Mapato ya sh bilioni 8.7. Inaeleza kuwa, kosa hili linahusu pia mamlaka ya TRA Ilala, ambao walihusika kufanya mauzo hayo. Akaunti ya kampuni ya VIP Engineering and Management (VIPEM),
ilifunguliwa na mmoja wa wabia wa IPTL, James Rugemalira, ambaye alikuwa
akimiliki asilimia 30 ya IPTL huku kampuni ya Mechmar Bhd ya Malaysia
ikiwa na hisa asilimia 70. Kutokana na kiasi hicho cha hisa, Rugemalira amelipwa kiasi cha dola
milioni 75 (Shilingi Bilioni 123), zikionyesha kwamba alilipwa kiasi cha
dola milioni 7.5 (Shilingi bilioni 12.4) mwaka jana na kiasi
kilichosalia alimaliziwa mwaka huu. Kiasi hicho cha fedha kililipwa kwa Rugemalira na kampuni ya PAP
inayomilikiwa na Harbinder Singh, ambaye kwa sasa ndiye mmiliki pekee wa
IPTL baada ya kununua hisa za Mechmar na zile za VIP. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo Gazeti hili imeinasa, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Gavana wa Banki Kuu
(BoT), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, walivunja sheria kwa kuelekeza
kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye tozo la uwekezaji isilipwe na
kusababisha serikali kupoteza mapato ya sh bilioni 21. “Waziri kwa kushirikiana na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini,
hawakufanya utafiti wa kini kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya
IPTL. Katibu Mkuu alisaini kutoa fedha za Escrow bila kuhakikisha fedha
za Tanesco zinarudi, hivyo kusababisha upotevu wa zaidi ya sh bilioni
321,” inasema sehemu ya ripoti hiyo. Kwa upande wa Tanesco, Mkurugenzi wa Shirika hilo na Bodi yake,
hawakutimiza wajibu wao kwa kugeuza maamuzi yao (ama kwa kushinikizwa na
Wizara au kwa rushwa), na kulikosesha shirika hilo zaidi ya sh bilioni
321. Wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikaririwa bungeni kwamba fedha hizo sio za umma, ripoti hiyo inaonyesha kuwa ni za umma. Mgogoro uliosababisha fedha kuwekwa katika akaunti hiyo ya Tegeta ya
BoT, ulitokana na Tanesco kugoma kulipa gharama za uwekaji mitambo
(Capacity Charge), kwa IPTL mwaka 2006 kwa vile ilibainika IPTL ilikuwa
ikitoza gharama kubwa kuliko iliyopaswa. Akaunti hiyo ya Tegeta, ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha
zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande
hizo mbili umalizike. Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya Nishati
na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada
ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina
ya wamiliki wa IPTL na Tanesco umemalizika na hivyo Benki Kuu haina
sababu ya kuhifadhi fedha hizo tena. Uamuzi huo wa kulipwa, ulizua upinzani mkali bungeni ambapo wabunge
wawili wa kambi ya upinzani; Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi),
David Kafulila na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe,
walidai kuwa zoezi hilo limejaa ufisadi na Bunge liliazimia kwamba suala
hili lifanyiwe uchunguzi wa kina na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja na ile ya Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru).