Bwana Allan Menas Lwambano anayedaiwa kumuua mkewe.
Hali huenda ikigeuka, wakati jamii inaamini akina baba ndiyo wenye tabia ya kutokuwa na uchungu kwa
watoto, imekuwa tofauti kwa mama huyu!Ni mkazi mmoja wa Kijiji cha
Mwanamonga, Kata ya Lilambo, Manispaa ya Songea, Kasiana Komba (60)
anadaiwa kuuawa na mumewe, Allan Menas Lwambano (76) kisa kikidaiwa
mambo ya kumtoa kafara mtoto.Tukio hilo la kuhuzunisha lilijiri usiku wa Agosti 25, mwaka huu ambapo
maelezo ya mume huyo yanasema ni baada ya marehemu kumtaka akubali
kumuua mtoto wao mmoja (jina tunalo) kati ya saba ili walipe madeni kwa
imani ya kishirikina na kufanikiwa katika kipato (utajiri).
Ilielezwa
kuwa, mwanaume huyo alikataa ombi hilo na mkewe akamwekea mgomo wa
kumnyima unyumba hadi pale atakapokubali ombi lake hilo.
Ilidaiwa
kuwa, maisha ya wawili hao yakawa ya ‘sitaki nataka’, mume akitaka
unyumba mke hataki kwa vile amemkatalia kumtoa mtoto wao kafara wakati
yeye mke alishawaambia wenzake (kwenye ushirikina) kuwa, ameamua kumtoa
mtoto huyo lakini baba yake hakutaka kufanya hivyo.
“Siku
ya tukio usiku, Lwambano alirudi nyumbani na kumkuta mkewe amelala,
alianza kumshikashika mwilini kuashiria alimhitaji faragha, ndipo mke
huyo alipotoka nje na kuchukuwa mchi wa kutwangia mahindi kwa lengo la
kumpiga mumewe
Kasiana Komba aliyedaiwa kumtoa kafara mtoto wake ili apate utajili.
“Mumewe aliuzuia, akamnyang’anya na kumpiga mkewe kichwani, alianguka palepale na kufariki dunia,” kilisema chanzo.
MUME AHANGAIKA KUUZIKA MWILI
Habari
za ndani zinasema kuwa, mume alipobaini ameua aliuchukuwa mwili wa
mkewe na kuupeleka nyuma ya nyumba ambako kuna choo na kuuzika hukuakipanda migomba juu ili kuzubaisha watu.
WATOTO: “BABA, MAMA YUKO WAPI?”
Agosti 26, mwaka huu,
siku moja tu baada ya tukio hilo la kutisha, watoto ambao wanaishi
mbali na nyumba hiyo walifika na walipoona hawamuoni mama yao,
walimwuliza baba yao: “Baba, mama yuko wapi?” akawajibu: “Mama yenu
ameenda mjini Songea, atarudi.”
WATOTO WAENDA KWA MGANGA
Ikazidi kudaiwa kuwa, Agosti 27, mwaka huu,
watoto hao hawakukubaliana na majibu ya baba yao, wakaenda kwa mganga
wa kienyeji (jina halikupatikana mara moja) kwa lengo la kupiga ramli
ili kujua alipo mama yao.
Waombolezaji wakiwa msibani.
“Mganga
baada ya kuangalia ‘king’amuzi’ chake aliwaambia kama wanataka kujua
mama yao alipo, warudi wakamchukue baba yao na kumfikisha kwa mganga
huyo kwani yeye (baba) ndiye ana siri nzito.
“Watoto
hao wakiongozwa na kaka yao mkubwa (Mathias) walimpa baba yao maagizo
ya mganga. Ndipo baba huyo naye akawaambia kama wanataka kujua ukweli wa
mama yao alipo, waongozane hadi kwa mtendaji wa kijiji akasimulie mbele
yake.
MBELE YA MTENDAJI
Septemba 4, mwaka huu,
familia hiyo ikiongozwa na baba mtu walifika kwa Mtendaji wa Kijiji cha
Mwanamonga, Said Mango na Mwenyekiti wa Kijiji, Maria Kahimba ambapo
katika maelezo yake , mzee huyo alikiri kumuua mkewe kwa kumpiga na mchi
kichwani.
NUKUU YA MUME
Mzee huyo ananukuliwa hivi: “Nimemuua mke wangu nikamfukia nyuma ya nyumba yangu kwenye choo (watu wakapigwa butwaa).
Polisi wakiwa eneo la tukio.
“Sababu
kubwa ya chanzo cha tukio ni mke wangu nilimkatalia ombi lake la kutaka
tumuue mtoto wetu mmoja ili alipe madeni ya uchawi na kufanikiwa
kimapato.
“Nilimkatalia,
akawa ananinyima unyumba. Siku ya tukio nilimlazimisha kunipa unyumba,
akakataa akataka kunipiga na mchi, nikamuwahi yeye na kumpiga, akakata
roho.”
NANI ANAYEJUA?
Mwanamke
mmoja aliyekataa kutaja jina lake, aliliambia Uwazi kwamba, marehemu
aliwahi kumlalamikia kuhusu mumewe kugoma kumtoa mtoto wao mmoja kafara
ili waweze kupata mali. Alisema mumewe haoneshi kutaka mabadiliko.
“Alisema
namwambia mume wangu tumtoe mtoto mmoja kafara tupate utajiri lakini
alisema sitaki kusikia habari hizo, kwani yeye ameridhika na ufukara,”
alisema mwanamke huyo akimkariri marehemu.
POLISI WAFUKUA MWILI, WAKUTA UMEHARIBIKA
Baada
ya maelezo ya mzee huyo, vilio vilitawala, hakuna aliyeamini kisha
familia kwa kushirikiana na wananchi na jeshi la polisi,
RPC wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msekela.
walifika
nyumbani kwa mzee huyo akaonyesha sehemu aliyomfukia mkewe, polisi
wakaamuru mwili huo ufukuliwe ukakutwa umeharibika vibaya, hasa sehemu
ambazo mchi ulipiga.Baada ya polisi na madaktari kuufanyia uchunguzi
mwili wa marehemu, waliwaruhusu wanandugu wauzike. MTUHUMIWA YUKO
POLISIKamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Mihayo Msikela (pichani),
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na
jeshi la polisi kwa ajili ya taratibu za kisheria.
No comments:
Post a Comment