Monday, October 20, 2014

DIAMOND PLATNUMZ, KUFIKISHWA MAHAKAMANI SARE ZA JESHI ZAMPONZA

MSANII nyota wa muziki wa Bongo Flava nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ huenda akaingia matatani baada ya juzi kupanda jukwaani kutumbuiza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 akiwa amevaa sare ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kinyume cha sheria.
Tangu msanii huyo afanye hivyo, mjadala umeibuka kwa wengi wao kujiuliza nini maana yake na kama alifanya hivyo kwa kibali maalumu au la, hasa ikizingatiwa ni hivi karibuni Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wasanii na wengineo kutotumia mavazi hayo.
Mbali ya Diamond, hata vijana wake nao walishambulia jukwaa wakiwa katika mavazi hayo, akiwemo msanii aliyemshirikisha katika moja ya nyimbo zake, Ney wa Mitego.
Wakati shoo hiyo ikiendelea, baadhi ya mashabiki walianza kumzomea kila alipoimba kabla ya video kubwa ambazo zilikuwa mbele ya jukwaa hilo kuanza kuonyesha picha za mnato na video za mwanamuziki huyo akiwa amevaa mavazi hayo huku akiwa kama askari ‘anayekoki’ risasi katika katika bastora na baadaye katika bunduki ya kivita.
Kitendo hicho, kilionekama kuwakera zaidi maelfu ya wapenzi na mashabiki wa muziki waliokuwa wamejazana katika viwanja vya Leaders Club, huku kila mmoja akiwa na tafsiri yake.
Baada ya tukio hilo la juzi usiku, kitendo cha nyota huyo kuvalia mavazi hayo ya JWTZ, kimeibua mjadala hadi katika mitandao ya kijamii kuanzia jana asubuhi, ambapo picha za msanii huyo zikitumika kujenga hoja ya uhalali wa kufanya hivyo, huku vijana kadhaa wanaokutwa nazo mitaani wakiteswa vibaya na jeshi hilo.
Kwa upande wake Diamond, alitoa taarifa ndefu katika ukurasa wake wa Facebook na Instagram, akiishia kuelezea ni kwa nini alizomewa katika shoo hiyo.
Tanzania Daima ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura juu ya kitendo cha msanii huyo, alisema alikuwa hajui chochote na kuahidi kulifanyia kazi kama atapelekewa taarifa na wasaidizi wake.
Alipotafutwa Kaimu Msemaji wa JWTZ, Meja Joseph Msanja, simu yake iliita bila kupokelewa na alipotafutwa msaidizi wake, alikiri kupata taarifa na kujionea kupitia shoo hiyo, huku akisisitiza bosi wake anaweza kulizungumzia hilo.
Tukio hilo limefanyika ikiwa ni siku chache tu tangu kijana mmoja aliyekuwa amevalia mavazi ya kijeshi maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam, kuvuliwa na kupewa adhabu ya kuogelea katika dimbwi la maji machafu yaliyotuama.
Aidha, msanii Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’ aliwahi kuhojiwa na Jeshi hilo kwa kutumia mavazi ya kijeshi katika kibao chake cha Simba wa Afrika, ambapo alijitetea pamoja na kuomba msamaha kwa kilichofanyika.
Kutokana na wimbi la watu mbalimbali hasa wasanii kuvalia mavazi yanayofanana na sare za jeshi hilo, hivi karibuni Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ, ilionya kama ifuatavyo:
Kumejitokeza kama fasheni kwa baadhi ya wasanii, hasa wanamuziki wa Bongo fleva, kurekodi video zao wakiwa wamevaa sare za jeshi kama vile suruali, viatu, fulana, kaptula, mabegi au kofia.
Inawezekana kwa namna moja ama nyingine, baadhi ya watumiaji wa sare hizo hawafahamu ni kinyume cha sheria ya nchi kukutwa nazo, ingawa kutokujua sheria bado sio utetezi mbele ya mahakama.
Mtu yeyote yule asiye na ruhusa ya kushona, kuuza au kuingiza nchini sare za jeshi, atakuwa ametenda kosa, kwa hiyo atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Katika uvaaji au uingizaji nguo, kama itatokea kwamba nguo hizo zinafanana kwa aina yoyote ile na zile za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, ikadhaniwa kuwa ni hizo, mtu huyo ana hatia na anastahili kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria zinazohusu sare za majeshi zilizopo

Saturday, October 18, 2014

KADI YA RAIS OBAMA YAKATALIWA


BO II
Rais wa Marekani Barack Obama amejikuta katika wakati mgumu baada ya kadi yake ya muamana (credit card) kukataliwa katika mojawapo ya migahawa iliyopo jijini New York.Obama amekiri kukutana na mkasa huo alipokuwa akizunguma na waandishi wa habari baada ya kusaini agizo la rais litakalotumika kama sheria ya matumizi ya kadi za muamana ambayo itasaidia katika kuzuia wizi wa kadi hizo ambao umekithiri nchini humo.

Akizungumzia mkasa wa kukataliwa kadi yake, Obama amesema alifika katika mgahawa mmoja na baada ya kuhudumiwa vitafunwa, mara baada ya kadi kuingizwa katika mashine iligoma kufanya muamana, ndipo alipohisi kuwa kuna namna kadi hizo ‘zinachakachuliwa’, hivyo akalazimika kutumia kadi ya mkewe Michelle Obama kufanya muamana huo.
Tatizo la wizi wa kadi za muamana limeathiri watu takribani milioni 100 kwa mwaka jana, ambapo kusainiwa kwa agizo hilo la rais wa Marekani kutasaidia katika kuhakikisha usalama wa huduma za muamana na pia kuanzishwa kwa huduma ya dharura mtandaoni itakayowahudumia watumiaji waliopoteza kadi zao.
Marekani ni moja ya nchi zinazotoa huduma za kadi ya muamana ambapo mtumiaji wa huduma hiyo anakuwa na uwezo wa kupata huduma za malipo ya baada kwa manunuzi ya bidhaa na huduma mbali mbali.

SMBA AISHIYE NA BINADAMU BILA KUMDHURU


Kipande cha filamu ya Roar kikimuonyesha Tippi Hedren mama wa, Melanie Griffith's akicheza na simba anayeitwa Neil.
Melanie Griffith's akiwa amelala na Simba huyo kitandani mwake.
Melanie Griffith's akicheza na Simba.
Simba anayejulikana kwa jina la Neil akiwa amelala ndani ya nyumba.
Simba akiwa ameshika mguu wa Melanie Griffith's wakicheza nyumbani kwao Los Angeles, Marekani.
Tippi Hedren akipozi na Simba huyo.

Akiwa na miaka 14 mtoto aliyetambulika kama Melanie Griffth raia wa Los Angeles, Marekani aliweza kuishi na simba.
Akizungumza na gazeti la LIFE, mama wa Melanie, Tippi Hedren alieleza kuwa ilikuwa mwaka 1971 kipindi hicho Melanie alikuwa na miaka 14 ambapo walikuwa wakiishi kama familia na simba.
Simba huyo aliyekuwa amefundishwa kuishi na binadamu chini ya mtaalam wa wanyama, Ron Oxley, alikuwa na uwezo wa kula mlo mmoja kwa siku ambapo alikuwa akila nyama kilo 13.
 “Nilikuwa napenda kwa jinsi Neil alivyokuwa akiishi na mwanangu, alikuwa akilala naye katika kitanda kimoja.”

“Siku moja niliingia katika chumba cha mwanangu na kumkuta Neil akiwa amelala na mwanangu huku mikono yake ikiwa kwenye mdomo wa Neil, sikuogopa kwani amefundishwa jinsi ya kujiheshimu, hutakiwi kumshika eneo la puani mwake ama kumshtua ghafla kwa mikono katika uso wake,” alisema mama yake Melanie, Tippi.

Tayari kuna filamu imeshatengenezwa itakayojulikana kama Roar ambapo ndani yake kuna Neil pamoja na Melanie. Itatoka hivi karibuni.
Neil kwa sasa ana miaka 84 na amesharudishwa katika mbuga za kuhifadhia wanyama lijulikanalo kama Shambala lililopo California, Marekani na wanamchukulia kama mnyama wa kufugwa.

HATIMAYE LADY JAYDEE AVUNJA MKATABA NA GARDNER!


HABARI mpya kutoka kwa mastaa wanaodaiwa kuvunjika kwa ndoa yao, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’, inasemekana wamevunja mkataba wa kuendesha Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar. 
Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’. Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wawili hao walidaiwa kufikia uamuzi wa kuvunja mkataba baada ya kuona ndoa yao inasuasua kutokana na migogoro.“Lady Jaydee au Jide alipoona mambo yanakwenda ndivyosivyo alimshauri Gardner wavunje
mkataba wa Nyumbani Lounge ili kila mmoja awe na businesses (biashara) zake. “Walimfuata mmiliki wa jengo, wakamwambia kwamba wanavunja, akawakubalia,” kilinyetisha chanzo makini. Chanzo hicho kilizidi kwenda mbali zaidi na kudai kuwa mgahawa huo kwa sasa unamilikiwa na mzungu. 
‘Lady Jaydee’ na Gardner G. Habash ‘Kaptaini’ wakati wakiwa pamoja. “Mgahawa kwa sasa unamilikiwa na Mzungu mmoja ambaye amenunua baadhi ya vitendea kazi walivyokuwa wakivitumia na Jaydee amekuwa akimsaidia mzungu huyo baadhi ya mambo kwa kuwa ni mgeni Bongo ila sasa Nyumbani Lounge itafunguliwa kwa jina jipya la M.O.G na Jaydee atafanya shoo ya ufunguzi kama msanii tu,” kilisema chanzo hicho. 
Baada ya kushibishwa maelezo hayo, mwanahabari wetu alimtafuta Jide bila mafanikio lakini Gardner alipopatikana, alijibu kwa kifupi.
“Siwezi kuzungumza chochote katika suala hilo.”
Jide na Gardner wanadaiwa kutengana na kila mmoja akiishi kivyake lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha.
 

WAZUNGU WAKUTWA WAMEKUFA CHUMBANI JIJINI DAR.


Moja kati ya majeneza yaliyohifadhiwa miili ya marehemu yakitolewa ndani ya chumba hicho.Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa wawili hao ambao walikuwa wakifanya kazi katika baa iitwayo Mashua iliyo ndani ya Slipway, huku mwanamke, aliyetajwa kwa jina la Hotsan, akiwa ndiye Meneja, walikutwa chumbani kwao wakiwa wamefariki baada ya kutoonekana kazini tokea Jumanne, siku ambayo Watanzania walikuwa wakikumbuka miaka 15 baada ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. 
WAZUNGU wawili ambao ni mume na mke wanaodaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini, wamekutwa wamekufa chumbani kwao katika nyumba waliyokuwa wakiishi maeneo ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatano hii.
Inadaiwa kuwa baada ya kutotokea kazini katika muda wa kawaida, wafanyakazi wenzao walijaribu kupiga simu zao za mikononi, lakini zote zilikuwa zikiita pasipo kupokelewa karibu mchana kutwa na hivyo kuwapa maswali mengi yasiyo na majibu. 
Siku iliyofuata, inadaiwa kuwa wafanyakazi wenzao walipojaribu tena kupiga namba hizo, simu zote mbili hazikupatikana
Jeneza lingine likitolewa ndani ya chumba hicho. Awali, walihisi huenda wenzao wameamua kuacha kazi baada ya kupata sehemu nyingine, lakini baadaye wakafikia uamuzi wa kuwafuatilia nyumbani kwao ili kujua kilichotokea. 
Walipofika, walikuta milango ikiwa imefungwa kwa ndani, kitu kilichowafanya waamini kuwa walikuwa ndani. Kwa kushirikiana na majirani, wafanyakazi hao waliamua kuvunja mlango wa chumba wanacholala wanandoa hao na kuwakuta wakiwa kitandani wamelala, kila mmoja akiwa amegeukia upande wake. 
Baada ya kuona tukio hilo la kushtusha, waliamua kuwaita Polisi ambao walipofika na kuiona miili hiyo, waliamua kuwaita wenzao wa kitengo maalum cha uchunguzi (Crime Investigation) ambao baada ya kufika, waliwataka raia na majirani waliokusanyika hapo kukaa mbali ili kuwapisha kufanya uchunguzi. 
Kamanda Suleiman Kova. Askari hao walikaa na miili ya marehemu kwa zaidi ya saa tatu wakiwafanyia uchunguzi na baada ya kukamilika kwa zoezi hili, miili hiyo ilichukuliwa kupelekwa hospitalini Muhimbili. 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja marehemu kuwa ni Roxxana Hilari na Hainess Hilton William na kwamba uchunguzi zaidi juu ya kilichowaua unaendelea.

NDEGE AGEUKA KUWA MWANADAMU

Kitendo hicho kiliwaacha wananchi vinywa wazi wasijue la kufanya huku wakibaki kupiga picha kwa kutumia simu zao za mikononi.Mapema wiki hii katika kijiji cha Oshindi nchini Nigeria wananchi walishuhudia sinema ya bure ambapo kamera zao zilikuwa macho yao na simu zao pale ndege aliyekuwa anapaa angani ghafla alianguka chini baada ya kudandia nyaya za umeme na kugeuka mwanamke.
Mwanamke huyo alionekana kuchubuka na kuwa na vidonda katika mwili wake hali iliyo kuwa inahuzunisha huku akiwa haongei (bubu).
Wananchi hao walimuuliza maswali mengi wakitaka kujua imekuaje hadi akageuka binadamu wakati yeye alikuwa ndege anapaa juu.
Mama huyo aliwajibu kuwa alikuwa anaenda kumtazama binti yake aliyekuwa amejifungua muda mchache.
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi na binti yake alikuwa anafanya sala wakati yule mama alikuwa anapaa. Inaelezwa kuwa wakati sala inaendelea ndipo mwanamama huyo aliyekuwa amejibadilisha na kuwa ndege akageuka binadamu.
Taarifa zinaarifu kuwa binti yake alikuwa kila akijifungua mtoto anafariki papo hapo.

Friday, October 17, 2014

MTANZANIA AWAUA WATOTO WAKE WAWILI KATIKA HALI YA KUSTAJABISHA HUKO AUSTRALIA

Raia wa Tanzania anayeishi katika jiji la Melbourne, Australia, Charles Amon Mihayo, 36, aliwanunulia binti zake Savannah, 4, na Indianna, 3, gauni za dance ya ballerina, akawaangalia wakidansi, kisha akawaua wote wawili kwa kuwakaba. 

Baada ya kuwaua mabinti hao, Mihayo aliwapigia simu polisi kuwataarifu, kisha aliiogesha miili ya marehemu, na wakati akiivalisha nguo miili hiyo, aliwaambia polisi waliofika na kugonga mlango, wasubiri kidogo.

Alipofungua mlango, polisi walimuuliza, kwanini amewaua watoto wake. Mihayo alijibu kuwa hakuna “good reason for what he did but it made sense to him at the time” [hakuwa na sababu ya maana ya kuwaua, lakini aliona ni kitu cha busara wakati anafanya mauaji hayo.]
savannah indianna Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Savannah,4, na Indianna, 3, enzi za uhai wao

Mtuhumiwa alisema kuwa hakupanga kuwaua binti zake, lakini hiyo haijalishi sasa maana maji yameshamwakiga; na kwamba hakutakiwa kufanya vitendo hivyo lakini ndio imeshatokea.


Dakika tisa baada ya Mihayo mwenyewe kuwapigia simu polisi na kuripoti kuwaua wanae, mama wa watoto hao aliwapigia simu ya dharura polisi kuwataarifu kuwa kuna kitu kimewatokea wanae waliokuwa wameenda kumtembelea baba yao.
Ripoti ya polisi inasema siku moja kabla ya tukio, Mihayo alimtumia text-message mama wa wanae, ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na watoto hao, kumuomba awapeleke watoto wakamtembelee ili awaone mara ya mwisho.

Kabla ya kukutana, Mihayo aliwanunulia watoto hao gauni na viatu. Mama na watoto walipofika nyumbani kwa Mihayo, apartment ambayo amepangisha kutoka kwa bibi wa wanae, Mihayo alimuuliza mzazi mwenza ana muda kiasi gani na wanae, kisha akawaingiza ndani.
charles mihayo Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Charles Mihayo ndani ya gari la polisi, akificha sura yake kutoka kwa wapiga picha

Mama na bibi waliwasikia watoto wakicheza, kabla ya mmoja wa watoto hao kutoka barazani akiwa amevaa gauni ya maua na viatu vyeupe alivyonunuliwa na baba yao.

Mtoto huyo alianza kudansi kabla ya baba yake kumuita arudi ndani, ili ajitayarishe kumuonyesha mama kitu kingine dakika kumi baadae.
Baadae kidogo, mama na bibi waliona watoto wamekuwa kimya. Mama aligonga mlango, Mihayo akamwambia asubiri kidogo. Mama huyo akagonga tena. Mihayo akafoka “utajua watakapofika hapa!” Akimaanisha polisi. Mama alikimbilia kwenye sebule ya mama yake na kuwapigia simu polisi. Polisi, ambao tayari walishapigiwa simu na Mihayo mwenyewe, walipogonga mlango, Mihayo aliwajibu “I’m just finishing up.”
savannah indianna mom Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Marehemu Savannah na Indianna, wakiwa na mama yao

Alipofungua mlango, huku akifuta mikono yake na taulo, aliwaambia polisi: “tayari nimemaliza…Nimeshawaua” [It's done, I've killed them.]
Mihayo, ambaye alikiri kuwaua watoto hao kwa kuwakaba baadae aliwaambia polisi kuwa alikuwa amefurahia mama watoto kuwaleta wanae, ili aseme “goodbye” kwao kwa mara ya mwisho. Mihayo aliwaeleza kuwa aliwavalisha wanae gauni za ballerina na mabinti wakaanza kudansi. “Walienda nje kumuonyesha mama yao nguo zao mpya” alisema Mihayo. Alisema kuwa watoto waliporudi ndani, alirekodi video na simu yake watoto hao wakidansi nyimbo ya “Let it Go” kutoka kwenye movie “Frozen.”
Mihayo alisema baada ya nyimbo kwisha, watoto hao walianza kucheza mchezo wa “hide and seek”(unafanana na kombolela.) Hapo ndipo alipoweka mto nyusoni mwa watoto wote wawili, na kuwabana mpaka walipoacha kuhangaika na kupumua.
charles mihayo 0 Jinsi Mtanzania alivyoua binti zake nchini Australia, katika hali ya kustaajabisha
Picha ya kuchorwa ya Charles Mihayo akiwa mahakamani. 

Camera haziruhusiwi mahakamani
Baada ya watoto hao kupoteza maisha, Mihayo aliwapigia simu polisi, na kuwapeleka watoto hao bafuni na kuanza kuwaogesha na kuwavalisha nguo.
Mihayo hakutoa sababu za mauaji hayo zaidi ya kusema wapelelezi hawawezi kuelewa “what he has been through” na kwamba kutoa sababu ya mauaji haitabadilisha chochote.

Mihayo anashikiliwa mahabusu, akisubili kutokea mahakama kuu kukabiliana na tuhuma siku za usoni.