Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mti aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii.
Na Mwandishi wetu Peramiho
Songea
Mwanaume mmoja Fredrick Mgaya (60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani
Ruvuma amejinyonga usiku wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo karibu na
viwanja vya michezo vya Abasia kijijini Peramiho.Mwanaume
huyo aliyekuwa akifanya kazi kitengo cha maabara katika Hospitali ya
Peramiho na kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa amejinyonga
majira ya asubuhi ya leo. Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye kujitoa uhai. Afande
Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa kwanza,anasema “
Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la wanafunzi wa shule
ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini wamesimama badala ya
kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu ananing’inia kwenye
mti pale.
Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee wetu Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
Ni
tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii ambaye
tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na migogoro yake na mkewe lakini
uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri kabisa.
Kama
mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi wajaribu kutafuta
suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa uhai”
Akiongea
Hakimu wa mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria Sambo amesema,
ameshaletewa na kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu mara mbili
na hadi sasa kuna kesi inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi,
lakini kwa hali ya kawaida hakudhani kwamba marehemu Fredrick Mgaya
angefikia hatua hiyo ya kujitoa uhai.
Nao
mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi wamelaani uamuzi
uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa watu na pia
alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla.
Uamuzi
ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan ndugu, jamaa pamoja na
marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye kwa mambo
mengi ya kimaisha.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani ameonesha masikitiko
yake ya dhati kwa kuondokewa na moja ya wazee aliokuwa akiwategemea kwa
ushauri katika kijiji chake.
“Tukio
hili linagusa sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na
ambaye tunashinda nae siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini
anakipanga katika akili yake”.
Ndoa
nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale, hivyo ni vizuri
watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii kujaribu kutoa
mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili kuepusha adha
kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii yetu.
Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi Kapinga.
Winfried
Thadei Mgaya, mdogo wa marehemu anasema, amepokea tukio hilo kwa
mshtuko na kwa majonzi sana. Anapata uchungu sana juu ya msiba wa kaka
yake kwani marehemu ameacha watoto wanne ambao bado ni tegemezi pamoja
na mjane. Pia amesema mazishi yatafanyika tarehe 7 jumamosi kijijini
kwao Madaba, Songea mkoani Ruvuma.Habari kwa hisani ya Demashonews
No comments:
Post a Comment