Watu wapatao
32 wameuawa katika maporomoko ya ardhi katika mkoa wa Hiroshima nchini
Japan.Maporomoko ya ardhi yametokea katika eneo la makaazi ya watu
karibu na mlima katika vitongoji vya mji wa Hiroshima.Maporomoko hayo
yamesababishwa na mvua kubwa zilizonyesha kwa saa 24 kuamkia Jumatano
asubuhi zikiwa sawa na kipimo cha mvua za mwezi mzima, limesema Mamlaka
ya Hali ya Hewa ya Japan.Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha nyumba
zikiwa zimefukiwa katika matope na miamba, wakati kikosi cha uokoaji
kikielekea nyumba hizo.
Watu wengine tisa bado hawajulikani walipo, limesema shirika hilo.
Afisa
mwingine wa serikali ya mtaa katika mji huo amesema "baadhi ya watu
wamechukuliwa na maji na ilikuwa vigumu kujua kwa uhakika idadi yao",
Shirika la habari la AP limesema.
Mwandishi wa habari wa BBC Rupert Wingfield-Hayes amesema wengi wa waliokufa ni watoto.
Mmoja
mwenye umri mdogo kabisa kufariki dunia katika tukio hilo ni mvulana
mwenye umri wa miaka miwili, Shirika la habari la Japan, Kyodo
limeripoti.
Miongoni
mwa waliokufa ni mfanyakazi wa uokoaji mwenye umri wa miaka 53 ambaye
amekufa baada ya udongo kuporomoka tena, shirika la Hali ya Hewa la
Japan limesema. Aliweza kuwaokoa watu watano wakati wa operesheni hiyo.
Maporomoko hayo yamelikumba eneo la makaazi nje kidogo ya mji wa Hiroshima magharibi mwa Japan
Mtu mmoja akiwa amesimama katika kifusi cha nyumba katika kisiwa cha Izu Oshima kusini mwa Tokyo Oktoba 16,2013
Matope na miamba ilizikumba nyumba kadha, na kuwaacha wakijihifadhi kwenye mapaa ya nyumba.
Wafanyakazi wa uokoaji wanawatafuta watu walionusurika lakini haijafahamika ni watu wangapi wamepotea.
Mmoja wa
walionusurika ameliambia shirika la AP: "Niliamka katikati ya usiku na
njia ya sehemu ya kuelekea chumba cha maongezi ilikuwa tayari imefurika
maji."
"nilisikia
sauti ya maji yakiingia, na hatimaye maji kutoka mtoni yaliingia ndani
ya nyumba yangu, kwa hiyo nilichukua gari na kuondoka."
Profesa mmoja katika chuo kikuu cha Hiroshima, JJ Walsh, ameiambia BBC kila mtu alishangazwa na kiwango cha upepo huo.
"Watu
wengi wamezoea mvua kubwa. Tuna msimu wa mvua. Lakini nafikiri kila mtu
alikutwa na hali hii bila kujitayarisha kwa kiwango cha mvua
iliyonyesha," amesema.
Waziri
Mkuu wa Japan Shinzo Abe amewataka maafisa wa serikali katika eneo hilo
kuongeza idadi ya wafanyakazi wa uokoaji ili kuimarisha operesheni ya
uokoaji".
Mvua zaidi zinaweza kusababisha maporomoko zaidi ya ardhi, wameonya maafisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.
Sehemu kubwa ya sehemu ya kati na kusini mwa Japan ni milima, huku nyumba nyingi zikiwa zimejengwa katika miteremko mikali.
Mwaka
uliopita, kimbunga kilisababisha maporomoko ya ardhi katika kisiwa cha
Izu Oshima, kusini mwa mji mkuu wa Tokyo, ambapo watu 35 walikufa.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment