Meninah
habari mpya zinasema kuwa vikao vya harusi ya Diamond na Meninah
ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva vimeanza kimya kimya nyumbani kwa
mama Diamond huku mmoja wa wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond mwenyewe
na Queen Darling ambaye ni dada wa Diamond.
Habari ambazo zimezagaa kila mtaa ni kwamba msanii huyu ameamua kufanya mchezo mchafu huu kwa kuendelea kukamata masikio ya watanzania ili umaarufu wake usichakae. Wapo wanaodai ya kuwa mchezo aufanyao Diamond ni moja ya masharti ya watu waliojiunga na freemasons wakidai kuwa yawezakuwa aliomba nyota ya mvuto kwa mashabiki ili akubalike huku wakidai ndicho kilichtokea kwa jamaa huyu, hivyo wakifananisha na matukio ayafanyayo kuhusu yeye kuoa wakidai kuwa kama muoaji na aoe kuliko kuwababaisha wapenzi wake kila leo wakisikia leo yupo na huyu kesho na huyu kitu ambacho wamedai kuwa sharti la nyota hiyo ni kutokuoa.
wengine wakaunganisha na tukio la kanumba kuwa nae ilikuwa hivyo hivyo kuwa anaruhusiwa kuwa na mwanamke lakini sio mke na ndio maana Diamond anawechezea danadana wanawake wakitanzania wanaotaka kuolewa na wanaume maarufu kama yeye.
Na katika kufuatilia hili kuhusiana na harusi hii, mwandishi alienda nyumbani kwa
Diamond hivi juzi kati kufanya nae mahojiano hata hivyo hakumkuta
Diamond lakini alimkuta mmoja wa watu wake wa karibu ambaye yupo pia
upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema
bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya Diamond na Meninah na vikao vimeanza
kwa mama Diamond. Chanzo hicho kilisema kuwa Diamond na Meninah
walikutana takribani miezi mitano iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo
za Kili Awards 2014 ambapo wote walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia
mapenzini kimya kimya mpaka wiki za hivi karibuni gazeti moja
lilipovujisha habari hizo za mahaba ya Diamond na Meninah na media
nyinmgine kuziandika kwa kasi
No comments:
Post a Comment