Thursday, September 4, 2014

MUME WA KAJALA...AMUOMBA MKEWE AMTOE GEREZANI

Kajala na mumewe wakiwa mahakamani.

 
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo. 
 

Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla. 

Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa. 

Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.

No comments:

Post a Comment