Maafisa wa kanisa wanasema kuwa watawa hao waliuawa na mhali mwenye akili pungwani
Watawa watatu wakongwe wamebakwa na kuuawa mjini Bunjumbura katika makazi ya watawa wanawake viungani mwa mji mkuu huo.
Sababu
ya mauaji hayo haijulikani. Polisi wanasema kuwa wamewazuilia washukiwa
wawili, kulingana na shirika la habari la Reuters.
Watawa hao walisemekana kuwa Lucia Pulici,mwenye umri wa miaka 75, Olga Raschietti, 82 na Bernadetta Boggian, 79.
Wawili kati ya waathiriwa, waliuawa Jumapili huku mwili wa mwingine wa tatu ukipatikana Jumatatu ukiwa umekatwakatwa.
Maafisa wakuu wanasema kuwa mshukiwa wa mauaji hayo, alionekana akitoroka makazi ya watawa hayo akiwa ameshika kisu mkononi
Dayosisi ya Italia ya Parma inasema kuwa watawa hao waliuawa wakati wa jaribio la wizi katika makazi yao.
Hata hivyo haijulikani kwa nini watawa hao waliuawa kwani hakuna kilichoibwa kutoka kwao.
Watawa hao wawili walikuwa wanashiriki katika kanisa katoliki la Xaverian.Kwenye
mtandao wake, dayosisi ya kikatoliki ya Parma ilisema kuwa mauaji ya
watatu hao yalifanywa na mhalifu ambaye alikuwa na matatizo ya kiakili.
Mnamo mwaka 2011,mtawa mmoja na mfanyakazi wa shirika la misaada aliuawa katika tukio la ujambazi Kaskazini ya Burundi
Burundi ni moja ya nchi masikini ambapo uchumi wake unategemea sana mapato kutokana na Chai na Kahawa zinazouzwa nje
No comments:
Post a Comment