Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (katikati) na Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema wakimsikiliza miliki wa Nyumba ya
kulala wageni United State na bar, Laurent Kasiga iliyopo Mbagala Rangi
tatu, Dar es Salaam ambayo iliteketea kwa moto uliotokana na roli la
mafuta lililopinduka na kuwaka moto wakati vijana wakiiba mafuta.
Mkuu wa Moa akikagua Nyumba hiyo ya kulala wageni iliyokuwa na vyumba 32.
wananchi wakiangalia athari za moto huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiangalia tenki la lori hilo.
Lori hilo lilivyoteketea kwa moto uliosababishwa na mshumaa.
Moja ya maduka ya vifaa vya pikipiki lililoteketea
Wafanyabiashara
wa mchele waliokuwa na fremu katika eneo hilo wakiwa katika majonzi
baada ya mzigo wao kuungua moto na kuharibika kabisa.
Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo la moto akisimulia.
Baadhi ya sehemu za mwili za watu walioungua. Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akiwa na mmoja wa wauguzi wa
hospitali ya Temeke alipowatembelea waathirika wa ajali hiyo. WATU
watatu wamefariki na wengine sita wakiwa katika hali mbaya Hospitali ya
Muhimbili kufuatia tukio la moto uliolipuka kwenye gari la kubeba
mafuta jana maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
AKizungumza
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna Mohammed
Mpinga, alisema ajali hiyo haikuleta athari yoyote baada ya gari lile
kupata ajali ila athari ilijitokeza baada ya watu kuvamia na kuanza
kuiba mafuta na baadaye kujaribu kuiba betri ndipo cheche za moto
zilipolipuka na kusababisha kuwaka kwa gari hilo.
Wakati
huohuo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick, amewataka wananchi
kutokuwa na tabia ya kuvamia ama kuiba vitu pindi ajali zitokeapo.
Sadick alisema hayo alipotembelea hospitali ya Muhimbili na Temeke walipolazwa majeruhi hao.
No comments:
Post a Comment