Ulozi? Mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23),
anadaiwa kufukuzwa nyumbani kwao kufuatia kuchanganywa na penzi la
mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi aliyejulikana kwa jina moja la
Zein. Mrembo anayejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23)
anayedaiwa kufukuzwa nyumbani. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya
kutimuliwa kwao, binti huyo ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake walezi
maeneo ya Kariakoo jijini Dar alisimulia kwamba alifukuzwa kwao kwa
sababu hakulala nyumbani siku moja wiki iliyopita na aliporudi wazazi
wake walezi wakamtaka arudi alipotoka.
“Baada ya kufukuzwa sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kuja
kwa mpenzi wangu (Zein) maana ninampenda na siku si nyingi atanioa.
Mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi anayejulikana kwa jina moja
la Zein. “Mama na wajomba wameshakubaliana na uamuzi wangu isipokuwa
baba tu,” alisema binti huyo.
Alipotafutwa mganga huyo mwenye maskani yake Magomeni-Mwembechai,
Dar, alisema kwamba ni kweli yupo na binti huyo na lengo lake ni kumuoa.
No comments:
Post a Comment