Kama ilivyokawaida kwa mashindano mengine watanzania kuwa
wasindikizaji na washuhudiaji wa wengine kuchukua tuzo huku wao wakiambulia
patupu, kwao Brothers For Christ imekuwa tofauti baada ya kuchukua tuzo katika
mashindano ya PRAYZ FACTOR PEOPLE CHOICE AWARDS nchini Marekani.
Kundi hilo ambalo maskani yake ni Tegeta jijini Dar es
salaam lilifanikiwa kuchukua tuzo mbili katika Afro category na International
Category na kuwaacha watu kuachwa na mshangao huku wakiwa hawaamini
kilichotokea. Tamasha hilo lilifanyika tarehe 22/9/2014 lilifanya nyimbo za B4C
kupigwa sana na vituo vya media nchini marekani na kulifanya kundi hilo
kujizolea mashabiki wengi nchini humo kitu ambacho ni tofauti na hapa Tanzania.
Brothers for Christ walijaribu kutupa kete yao huko baada ya
kuona tangazo katika mtandao kuwa kuna mashindano hayo ndipo walipotuma Video
yao ya YOTE YAWEZEKANA ili ichaguliwe kuingia katika mashindano hayo.
Waswahili husema
“kama bahati vile” wimbo huo ulichaguliwa katika vipengele viwili
ambavyo nao waliwaonyesha wamarekani na wahudhuriaji wote ya kuwa hakika Yesu
Kristo anahubiriwa Tanzania kupitia nyimbo.
"Tulipokuwa tumepanda jukwaani watu walionekana kuwa na
mshangao wakiwa hawaamini kile kilichokuwa kinatokea baada ya umahili na ustadi
tuliouonyesha katika kuimba live, wengi walituuliza tulipotoka tukawajibu
Tanzania wakashangaa" alisema Justin Kaego
Kundi hilo ambalo
liliiwakilisha vyema Tanzania halina jina kubwa nchini lakini
limefanya mambo makubwa yakushangaza kwani wapo wanamuziki wakongwe waliowahi
kushiriki katika mashindano kama haya na hawakuweza kurudi na tuzo.
Brothers For Christ (B4C) ni kundi la vijana 14 wakiwemo
watanzania 8, wakenya 2 na wacongo 4 ambao wameunda kundi hilo likiwa chini ya Dockta
Mponzi ambaye pia ni mzee wa kanisa la Mlima wa moto Asseblise of God Mikocheni
Dar Ambaye ndiye mlezi wao. Ni vijana wasiojua kuimba kwa kutumia mshindo
nyuma, wenyewe husema “ live bila chenga”.
Wapo tayari kwa mialiko ya aina yoyote kwani nia yao kuu ni kukiokoa
kizazi cha watanzania kupitia uimbaji. Hivyo wasiliana nao kwa +255767600604 na
+255753599542 wapo tayari kwenda popote kwa ajiri ya Kristo Yesu.
No comments:
Post a Comment