Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.
Magari nayo yameteketezwa kwa moto.
WAANDAMANAJI
nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga
kupitishwa kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore
kuongeza muda wa kukaa madarakani.
Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo.
Taarifa
kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama
tawala na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and
Progress yamechomwa moto pia.
Bunge hilo
lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia
madarakani tangu mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani.
Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao.
Kabla ya
kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua mabomu ya machozi kuwazuia
waandamanaji waliokuwa wakielekea katika jengo la bunge hilo japo
takribani watu 1,500 walifanikiwa kupenya na kulichoma bunge hilo.
Waandamanaji
walionekana wakichoma nyaraka na kupora baadhi ya vifaa vya kompyuta
huku magari yaliyokuwa nje ya jengo hilo nayo yakichomwa moto.
No comments:
Post a Comment