Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, msala huo ulijiri juzikati nyumbani
kwa ticha huyo, Kichangani ambapo mwalimu huyo alidaiwa kufumwa na mume
wa mtu, Raphael Bernard (33) ambaye ni dereva wa bodaboda.
KATIKA
hali ya kutisha, fumanizi lililoambatana na bonge moja la mtiti
linadaiwa kujiri nyumbani kwa mwalimu ‘ticha’ wa Shule ya Msingi ya
Mafisa ‘A’, iliyopo Manispaa ya Morogoro mjini hapa aliyefahamika kwa
jina la Rosemary Mkoba kisha watu wakachomana visu.
Habari
zilidai kwamba mwenye mume amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu,
akagundua huwa anakwenda kujichimbia kwa ticha huyo huku akiacha familia
ikilala njaa.
Ilisemekana
kuwa, siku ya tukio, mwenye mume, akiwa na ‘jeshi’ lake, alimfuatilia
mumewe hadi akamuona akiingia nyumbani kwa hawara wake huyo.
Ikazidi
kudaiwa kwamba baada ya kuhakikisha jamaa amelala kwa ticha huyo,
mwanamke huyo na ‘skwadi’ yake waliondoka, asubuhi iliyofuata mishale ya
saa 1:04 wakatia timu na kulianzisha timbwili huku mke huyo akidaiwa
kumtishia ticha kuwa akipata ujauzito atazaa kwa mdomo.
MASHUHUDA SASA
Nao
mashuhuda ambao ni majirani wa mwalimu huyo, Juma Hamis na Joyce Joseph,
walipozungumza na paparazi wetu walisema siku hiyo walisikia vurugu
kutoka ndani kwa mwalimu ambapo walikwenda kushuhudia.
Walisema
walimkuta mwanaume huyo akipigana na ticha ambaye alikuwa akiendelea
kulalamika kufichwa suala la mwanaume wake kuwa na mke.
WACHOMANA VISU
“Unaambiwa mzozo huo ulipamba moto, maana yule mke aliyeondoka alidai amemfumania mumewe, mwalimu naye akadai alikuwa hajui.
“Katika purukushani hiyo huku wakipigana wao kwa wao ndipo wakachomana visu. Yaani mwanaume alijeruhiwa vibaya mno.
HOSPITALINI
Baada ya
kuzungumza na majirani na mashuhuda wa tukio hilo, mwanahabari wetu
alitia gia kwenye pikipiki yake aina ya ‘boksa’ hadi Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa wa Morogoro.
Mwandishi wetu alizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk. Francis Semwene ambaye alikiri kuwapokea majeruhi hao.
“Mwanaume
alikuwa amepasuka tumboni hivyo tunaendelea kumpa matibabu, yupo wodi
namba moja na mwanamke ambaye naye amechomwa visu sehemu mbalimbali za
mwili wake, naye tunaendelea kumpatia matibabu,” alisema Dk. Semwene.
HUYU HAPA MWANAUME
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa tabu huku polisi wakiwa wamempiga pingu kitandani, Raphael alisimulia kwa maumivu makali:
“Mwezi wa tano mwaka huu, tuligombana, niliondoka nyumbani, kwa heshima ya mtoto wangu, sikuchukua kitu chochote zaidi ya nguo.
“Mwezi
huohuo nilifanikiwa kuingia kwenye uhusiano na Mwalimu Rosemary ambapo
baada ya penzi kukolea aliniambia nihamie kwake ili tulifaidi penzi letu
tamu yaani mahaba motomoto na niliishi pale miezi mitano.”
FUMANIZI?
Alipotakiwa
kuelezea chanzo cha tukio la fumanizi, jamaa alifunguka: “Hamna. Ticha
aliniamsha asubuhi akaniambia nimsaidie kufanya usafi na kumuogesha
mwanaye.
MADAWA YA KIENYEJI
“Nilipomaliza kumuogesha nilitaka kutandika kitanda, nilipoinua godoro niliona madawa ya kienyeji.
“Nilipomuuliza mwenzangu akawa mkali kama pilipili ndipo ugomvi mkubwa ukaanzia hapo.
“Baada ya mzozo mkali, ndugu zake walinivamia, akiwemo shemeji yangu wa kiume, namfahamu kwa jina la baba Dickson.
MAUMIVU
“Wakati najitetea, nilishika kisu ambapo katika hekaheka ya kunyang’anyana na Rosemary kilinichoma mimi na yeye.”
TICHA ARUHUSIWA
Mwandishi
wetu alifika wodi namba tatu aliyolazwa ticha huyo na kuelezwa kuwa
aliruhusiwa baada ya kupata nafuu ya majeraha mengi ya visu aliyoyapata
sehemu mbalimbali za mwili wake hasa kichwani.
Baada ya kumkosa ticha huyo wodini, gazeti hili lilimfuata nyumbani kwake, alipobanwa alisema:
”Tukio
hili limetokana na ushirikina wa mke wa zamani, alinitishia kuwa
nikishika mimba nitajifungulia mdomoni akiapa kunifanyia kitu mbaya.
“Yaani hata sijui nini kimetokea, Raphael, mume wangu kipenzi amenichoma kisu na yeye kujichoma tumboni.”
KAMANDA WA POLISI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Leonard Paul alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio
hilo liliripotiwa Oktoba 27, mwaka huu, ambapo Raphael alikwenda kwa
mpenzi wake, Rosemary ambako kulitokea ugomvi, wakaumizana kisa wivu wa
kimapenzi, hivyo tunamshikilia mwanaume huyo huku uchunguzi ukiendelea,”
alisema Kamanda Paul.
No comments:
Post a Comment