Saturday, November 1, 2014

VICTOR MBAGGA MWANAMUZIKI WA INJILI ALIYEPANIA KUWAKOMBOA VIJANA WA TANZANIA .



Ni kijana mwenye makao yake mwanga mkoani kirimanjaro na alianza huduma ya uimbaji mwaka 2002 huku akiwa na nia ya kukiokoa kizazi cha vijana wasiojiweza.
Brother Victor Bagga kama anavyojulikana ameamua kujitolea kufanya kazi ya kumtangaza Kristo kwa watu ili kuwaweka huru waliofungwa kama lisemavyo neon la Mungu.
“ Nina mzigo mkubwa sana  moyoni mwangu wa kutaka wasiojiweza wajue kuwa wanatumaini kwa Yesu na si kwa mwanadamu, wapo vijana wengi sana wanamaisha yakusikitisha kisa hawajui yakuwa Kristo Yesu ndio tumaini kuu 
Kujitambua kwa kijana ni kitu muhimu sana lakini vijana wengi wameshindwa kujitambua kwa kuwa wanaishi nje ya mpango wa Mungu. " Ukishajua umezaliwa ili ufanye nini huwezi kuhangaika sana na dunia ila shetani hataki vijana wajitambue matokeo yake  amewatwisha mizigo mikubwa na ndio wanaoongoza kwa kilio cha maisha magumu." alisema Brother Victor


Pia alisema huwa anatumia kipaji chake cha uimbaji kuwatia moyo watoto watogo na walemavu kwani ni makundi ambayo yamesahaulika sana katika jamii yetu. "ukweli ni kwamba ukifanikiwa kuyafanya makundi haya yakatambua vipaji vyao mapema na wakavitumia kwa usahihi hawatahangaika kutafuta kazi za kuwainua kiuchumi, kwani kipaji cha mtu na elimu ndio njia pekee ya kumuondolea mtu umaskini kuliko kusubiri ajira kutoka kwa mtu mwingine kitu ambaho ni kilio kikubwa kwa vijana.


 



 

Hata hivyo anafurahia kuwa chini ya uangalizi wa kanisa la Mount Zion church kwa mchungajji H. Kimario ambaye amekuwa msaada mkubwa sana kwake katika huduma zake ili kuweza kutimiza maono yake ambayo ni kuwa mwimbaji wa kimataifa na kuweza kusaidia vijana wenye kupoteza mwelekeo wa ndoto zao haswa katika uimbaji na watoto walemavu.
 

 Brother Victor amesema katika huduma yake zipo changamoto ambazo akifanikiwa kuzitatua ataweza kuwahudumia vijana wengi ili nao waweze kuwasaidia wenzao


"Natamani sana huduma hii iwe ya kimataifa na itawezekana ikiwa nitaungwa mkono na watu wote kwani hatuwezi kuuondoa umaskini kwa makundi haya kwakuwa ni watu wasio na kitu na hata maandiko yanasema "asio na kitu hatapewa kitu na hata aliye na kidogo hicho nacho hunyang'anywa hupewa aliyenacho" hivyo nilazima tuwasaidie watu hawa kujua vipaji vyao pia ili viwasaidie wawe na kitu ili wapewe kitu" alisema Victor

Hivyo anaomba kuungwa mkono na watu wote katika kufanikisha maono yake na changamato hizo ni pamoja na vifaa vya Muziki, pesa pamoja na mahali pa kuwatunzia vijana hao kwani wengi hawapo mahali pamoja.

Victor Mbagga kijana mwenye asili ya Tanga ana albam mbili mpaka sasa na  anatarajia kuzizindua zote kwa mpigo mwezi ujao na anatamani sana kama atapata nafasi ya kufanya kazi pamoja na Christina Shusho, John Lisu pamoja na Upendo Kirahilo kwani ndio miongoni mwa waimbaji ambao wamekuwa kivutio sana kwake na kusaidia kukuza kipaji chake cha uimbaji. "ipo siku nitawashirikisha waimbaji hawa katika nyimbo zangu nasubiri kibali toka kwa Mungu tuu" alisema

Yupo tayari kwa mialiko popote duniani ili kuzidi kumtangaza Kristo Yesu. Mpigie +255766480206

 

No comments:

Post a Comment