FUNDI AJINYONGA
Emmanuel
Carlos enzi za uhai wake. Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba,
kwa muda mrefu, marehemu alikuwa na mgogoro usioisha na mkewe Mariamu
Suleimani uliosababisha wawili hao kulala katika vyumba tofauti ndani ya
nyumba yao. Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kutokana na ugomvi
huo, marehemu alikuwa akirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na kumtukana
matusi mkewe huku baadhi wakienda mbali na kudai alikuwa haachi hela ya
matumizi.
hali ya kushangaza, mtu mmoja ambaye ni fundi seremala aitwaye
Emmanuel Carlos, mkazi wa Kwabinyau Magomeni jijini Dar amekutwa akiwa
amejinyonga saa mbili asubuhi Septemba 23, mwaka huu katika kile
kinachodaiwa kuchoshwa na mgogoro wa kifamilia.
Hata hivyo, mkewe marehemu anadaiwa kuwa na biashara yake ya samaki
na alikuwa akijituma ili kuhakikisha anapata nauli ili arejee nyumbani
kwao.
Mke
wa marehehu akilia kwa uzuni. Kwa mujibu wa maelezo yaliyopatikana, mtu
wa kwanza kujua kuhusu suala hilo alikuwa ni kijana wake mwenye umri wa
miaka saba, Celestine Carlos aliyekwenda chumbani kwa baba yake kuomba
hela ya shule, ambapo alimkuta akining’inia kwenye dari baada ya kuwa
amejifunga kamba kwenye feni.
Akizungumza na waandishi wetu Mariamu alisema kuwa siku moja kabla ya
tukio, mumewe alirudi nyumbani na kumtukana huku akilia na kumwambia
kuwa atamkumbuka sana katika maisha yake na kwamba kabla ya kupambazuka
mmoja wao atakuwa amekufa.
“Siku iliyofuata alipoamka alinikuta naosha vyombo, akanitazama kwa jicho baya kisha akaenda chumbani kwake ambako alijifungia.
Baadhi
ya wananchi wakiwa eneo la tukio. Nusu saa baadaye alikuja mwanaye
Celestine na kuniomba hela ya shule, nikamwambia aende akachukue kwa
baba yake, alipoingia akarudi na kuniambia baba yake ananing’inia, jambo
nililoona kama utani lakini baadaye nilienda na kumkuta akiwa
amejinyonga,” alisema Mariamu huku akilia kwa uchungu.
Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Jumanne Mneka alikiri kufahamu
mgogoro wa familia hiyo na kusema walikuwa wakiwasuluhisha kila mara.
Polisi
wakiwa eneo la tukio. “Juzi kati tu tumetoka kuwapatanisha, nashangaa
leo saa mbili asubuhi napokea taarifa kuwa Emmanuel amejinyonga,
nimehuzunika sana,” alisema.
Majirani wakiwa wameshtushwa na kushangazwa na jambo hilo, waliungana
na wapita njia kwenda kushuhudia tukio hilo, hali iliyoufanya mtaa huo
usipitike kwa muda.
Waandishi wetu waliwashuhudia polisi wakifika eneo hilo na kuuchukua
mwili na kuupeleka katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya
uchunguzi. Marehemu ameacha mke na watoto wawili.
No comments:
Post a Comment