Tumepokea
picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami
ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi,
Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado
hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa
majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wetu alietuletea taswira hizi
kuhusiana na hali ya barabara hiyo.
''Kama
una safari ya kwenda Iringa-Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi
basi sitisha safari kwani njia inefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna
lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado
inawaka na inesambaa sehemu kubwa''
No comments:
Post a Comment