Wakati Tanzania ikijivunia kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa
uchumi, juhudi nyingi zinafanyika ili kuona msemo huu haupitwi na wakati na
kuendelea kumfanya mkulima kunufaika na kile anachokifanya. Wataalamu na
watafiti wanajitahidi kila kukicha kubuni kila njia kufanya kilimo cha Tanzania
kinainuka kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ili kufikia viwango vya
kimataifa kama zilivyo nchi nyingine.
Rijk zwaan ikiwa ni kampuni ya uzalishaji mbegu za mboga
mboga nchini, wameamua kutumia njia za kisasa kuwafundisha wakulima jinsi ya
kutumia mbegu za kisasa kwa njia ya mitandao ya kijamii ya Whats App na
Facebook ambapo wamekuwa wakiwahimiza wakulima kutumia kilimo cha green house
ili kuepukana na hasara zingine ambazo zingeweza kuepukika kwa kutumia kilimo
hicho. Na kwakutumia njia hiyo imewarahisishia wakulima kushare uzoefu na
mtaalamu kila wakati wanapohitaji msaada.
Kwa njia ya mitandao ya jamii tumefanikiwa sana, kwani kwa
sasa teknolokia imekwenda mbali sana kitu ambacho kinatusaidia sisi kukutana na
wakulima hata kabla ya kuonana nao ana kwa ana, na tumekuwa tukijivunia ubunifu
huu kwani tumeona mwitikio wa wakulima kupasahana habari kuhusu shirika letu na
bidhaa zetu wao kwa wao. Alisema Bwana Abel Kuley, meneja uzalishaji na maendeleo wa Rijk zwaan
Wakati tunaanza kuuza mbegu, tulianza na wakulima ambao wana ardhi lakini hawajui kitu cha kufanya hivyo tulianza kuwaeleza faida ya kilimo cha mbogamboga na namna ya kulima kilimo bora hivyo wale walioanza walianza kidogo kidogo lakini kila aliyeanza hakuna aliyejilaumu kuwa alifanya makosa kuingia katika kilimo hiki kwa kuwa wengi walijutia kwa nini hawakuijua siri hii tangu awali. Aliongeza Bwana Abel
Baadhi ya mbegu zilizooteshwa tayari kwa kupelekwa shambani
Wakati tunaanza kuuza mbegu, tulianza na wakulima ambao wana ardhi lakini hawajui kitu cha kufanya hivyo tulianza kuwaeleza faida ya kilimo cha mbogamboga na namna ya kulima kilimo bora hivyo wale walioanza walianza kidogo kidogo lakini kila aliyeanza hakuna aliyejilaumu kuwa alifanya makosa kuingia katika kilimo hiki kwa kuwa wengi walijutia kwa nini hawakuijua siri hii tangu awali. Aliongeza Bwana Abel
Naye Bwana Hearald Peeters Mkurugenzi Mtendaji wa Rijk zwaak alisema wao
wanatoa huduma ya mbegu za kisasa za mbogamboga kwa wakulima wadogo wadogo na
wakubwa pia. Lakini tumekubali kufanya shughuli hii sisi wenyewe kwa kuwafikia wakulima moja kwa moja kwani
tunajua kuwa wateja wetu wametofautiana maeneo yao ya kilimo kwa maana ya hali
ya hewa, udongo, pamoja na magonjwa ya mimea kutokana na eneo husika, hivyo
hatutaki kuwauzia wakulima mbegu kana kwamba wote wanatoka sehemu moja. Alisema
Hearald Peeters akiwa katika shamba la nyanya ndani ya Rijk Zwaan
Hearald Peeters akiwa katika shamba la nyanya ndani ya Rijk Zwaan
Kila wakati tunapopata mteja mpya huwa tunamuuzia mbegu zetu
lakini huwa hatumuachi hivyo hivyo kwani huwa tunamfundisha mfumo mzima wa
jinsi ya kuzilima na kuzihudumia mpaka atakapovuna. Hata hivyo huwa
hatumuuachii mkulima kuuza mwenyewe hivyo huwa tunatafuta masoko kwa ajilli yake
japo wakulima wetu huwa wanapata wateja kabla hata hawajavuna, hivyo huwa
tunapenda kumuhudumia mteja wetu na kumuacha akiwa na furaha na kwa mtindo huu
wamekuwa wakipashana habari na kuongeza kasi ya kutumia mbegu zetu na kwa
kufanya hivi wakulima wengi wamekuwa wataalamu wa kilimo hiki kwani huwa
wanajifunza kwa vitendo kwa kusaidiana na wataalamu wa Rijk zwaan. Alisema
Bwana Hearald
Hata
hivyo Rijk zwaani wanawasihi wateja wao kuwa hakuna kampuni ya usambazaji wa
mbegu waliyoingia nayo mkataba kwa kuuza mbegu zao kwakuwa wao wanatoa huduma
ya uuzaji wao wenyewe ili kuhakikisha mkulima anapata mbegu halisi kutoka kwao
Nae Enock Nanyaro mkulima wa kikundi cha parokia ya
familiaTakatifu, Njiro mkoani Arusha amesema tangu aanze kutumia mbegu za Rijki
zwaan hajawahi kujuta kwani mafunzo aliyoyapata baada ya kununua mbegu zao
yalimfanya kuvuna mazao mengi kuliko miaka yote aliyowahi kulima.
“Nawashukuru sana watu wa kampuni ya……. Maana wao
ndiowaliotupeleka Rijk zwaan na kutukutanisha na wazalishaji wa mbegu hizi
ambazo ndio nazitumia mpaka leo hii. Sikuwhi
kuwaza kuwa ipo siku moja nitakuwa mtaalamu wa kilimo cha kisasa lakini sasa
Rijk zwaan wamenifikisha hapa nilipo leo alisema Bwana Enock
Enock Nanyaro akionyesha mmea uliooteshwa miaka miwili nyuma na bado unazaa matunda bora na yenye afya ikiwa ni mmoja ya mmea wa mfano ambao huutumia kuwaonyesha wakulima wenzake ambao humtembelea ikiwa yeye huita ni maajabu ya mbegu za Rikjzwaan.
Renalda mlay wa Shant Town mjini Moshi Kirimanjaro, alikiri
kuwa hakuwa na ndoto ya kuwa na shamba nyumbani kwake kutokana na eneo
alilonalo, lakini mafunzo aliyoyapata kupitia Rijki zwaan aligundua ya kuwa
anaweza akalima mboga mboga katika eneo alilonalo nyumbani na akapata faida
kitu ambacho anakifanya sasa.
“Mimi nalima pilipili na nyanya kwenye green house nyumbani
kwangu na ninapata faida mpaka watu wananishangaa. Nimeifanya hii ni ajira
yangu baada ya kuacha kazi ya benki kwani kiwango cha pesa ninachozalisha kwa
hili shamba ni zaidi ya mishahara ya baadhi ya watu wanayopata makazini.” Bi
Renalda alisema
“Nikianza kueleza uzuri wa mbegu hizi unaweza ukaacha kazi na
kuwa mkulima, kwani ukinunua mbegu za hii kampuni na kuziweka shambani hakuna
hata moja ambayo haitaota,na uzaaji wake ni maajabu sana.” Alisema Bwana Deo
Ryoba wa Moshono, Arusha
Bwana Ole Ngao yeye ni afisa kilimo wilayani simanjiro
alisema kuwa wakulima wasilaumu kuhusu uzalishaji duni wa mbegu za kisasa
tofauti na vile zinavyosifiwa isipo kuwa wanapasa kuilaumu serikali kwani ndio
iliyoshindwa kutoa elimu ya kilimo kwa wananchi wake. Pia alisema kuwa wananchi
wengi hawazingatii kile wanachoshauliwa na wataalamu wa kilimo kuhusu kilimo
cha kisasa.
“zipo teknolojia nyingi sana ambazo zinatumika sasa katika
kilimo, hali ya hewa na mabadiriko katika udongo yanayotokana na matumizi yamda
mrefu kwa kilimo yanamlazimu mkulima
kuenenda na sayansi na teknolojia ili kupta faida katika kilimo” alisema Ole
Hili ni jambo la
kujifunza kuwa elimu kwa mkulima yaweza kutolewa hata kwa mitandao ya kijamii. Ipo
haja ya mkulima kubadiri mfumo katika
kilimo kwani kwa hali ya sasa teknolojia inatumika kila mahali.
Pia serikali yetu ni lazima iunge mkono teknolojia ya kisasa
katika kilimo kwani kumuhubilia mkulima kuhusu mabadiriko ya hali ya hewa bila
kumwambia njia sahihi ya kuikabili ni kazi bure.
Hivyo basi ipo haja ya serikali kuitazama sera kwa jicho la
tatu ili kuondoa zile sharia zinazowabana watafiti wa kilimo katika kukuza
teknolojia katika kilimo Tanzania.
Rijk zwaani ni kampuni ya utafiti na uzalishaji mbegu za
mbogamboga iliyopo Usa mkoani Arusha, iliyoanzishwa mwaka 2008 na nia ya kuanzishwa
kwa kampuni hii ni kuboresha begu za mbogamboga ili kukuza kipato kwa mkulima wa kawaida kwa kushirikiana na mashirika mengine ya kilimo hapa nchini ikiwa ni SEVIA,
AVRDC, TAHA na wakulima wenyewe.
Kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao wamekuwa wakifanya
mafunzo kwa vikundi vya wakulima pamoja na kushiriki katika maonyesho ya
wakulima yanayofanyika kila mwaka hapa nchini na hata kushiriki maonyesho kama
hayo yanayoandaliwa na baadhi ya wadau wa kilimo nchini.
Hearald Peeters akifafanua teknolojia mpya ya kilimo kifaacho kwa watu wasio na ardhi kwa waandishi wa habari walipotembelea Rijk zwaan Arusha