Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono
baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa
kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya
kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed
Janabi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepumzika kwenye hoteli maalumu
baada ya kutoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore
Maryland alikotolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wa
Tezi Dume wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena
hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na
ushauri.
No comments:
Post a Comment