Katika
hali isiyokuwa ya kawaida na kusikitisha mbunge wa Jimbo la Busanda
mkoani Geita Lolena Bukwimba kupitia Chama cha Mapinduzi amejikuta
akitoa machozi baada ya kukuta wanafunzi wakike zaidi 25 wa shule ya
sekondari Nyakamwaga wakilala chini kwa kukosa vitanda.
Hali
hiyo imejitokeza jana wakati mbunge huyo akikagua miradi ya visima 6
vya maji anavyojenga katika kata ya Nyakamwaga wilayani Geita mkoani
Geita kwa kushirikiana na wananchi.
Mbunge
huyo alipomaliza kutembelea miradi hiyo alitembelea bweni la wasichana
wa shule ya sekondari Nyakamwaga na kujionea hali na adha wanayoipata
watoto hao wanaolala chini na kujikuta akibubujikwa machozi.
Kufuatia hali hiyo ngumu ya maisha ya wanafunzi hao,mbunge huyo aliahidi kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya kununua vitanda na mahitaji mengine na kuwaomba wahisani na wafanyabishara wengine kusaidia shule hiyo.
Kufuatia hali hiyo ngumu ya maisha ya wanafunzi hao,mbunge huyo aliahidi kiasi cha shilingi milioni tano kutoka kwenye mfuko wa jimbo kwa ajili ya kununua vitanda na mahitaji mengine na kuwaomba wahisani na wafanyabishara wengine kusaidia shule hiyo.
''Jamani
mimi kama mbunge wa jimbo hili nimeona hali ilivyo mbaya kwa wanafunzi
wa kike wanavyoteseka sina cha kuongea nawaomba wahisani na
wafanyabishara tuungane kusaidia jambo hili'' alisema Bukwimba
''Hatuna
vitanda tunalala chini na magodoro ni machache uzio hakuna tunaoga
usiku kwa kuogopa wananchi wanaopita hata walimu wetu wanaishi watatu
hadi wanne kwenye chumba kimoja kwa kweli tunateseka sana tunaomba
tusaidiwe'' walisikika wakisema mwanafunzi hao.
Mkuu
wa shule hiyo Meryciana Deusdedith alisema kuwa shule yake yenye
wanafunzi 319 wakike wakiwa ni 188 na wavulana wakiwa ni 131na walimu 18
imekuwa na changamoto nyingi kama kukosa maabara na kukosa uzio jambo
ambalo watoto wakike wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi kwa kuogopa kubakwa
wakati wa kuoga.
Aliongeza
kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa wakianza wengi lakini kutokana na
shule hiyo kukosa mabweni ya kutosha wamekuwa hawamalizi kutokana na
kurubuniwa na vijana wa mitaani kwa kuwapa mimba na kuwakimbia na
kubaki wakihangaika.
Hata
hivyo alitoa shukrani zake kwa mbunge kwa kuona hilo na kuweza kusaidia
kiasi hicho cha fedha na kuwaomba watu wengine kusaidia shule hiyo kwa
chochote walichonacho.
No comments:
Post a Comment