Mtoto
mwenye umri wa miaka 8 anayedaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake. Tukio
hilo la kushangaza lililonaswa na Ijumaa Wikienda lilijiri wiki
iliyopita mishale ya saa 8:00 mchana maeneo ya Majengo Mapya, Kata ya
Kihonda jirani na nyumbani kwa aliyekuwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya
Bongo, marehemu Alberth Keneth Mangweha ‘Ngwea’.Hatari! Mtoto wa kike
mwenye umri wa miaka 8 (jina linahifadhiwa kimaadili), mkazi wa Kihonda
mjini hapa anayesoma darasa la kwanza kwenye Shule ya Msingi Noto
Sosario, anadaiwa kutumika kumwiba mtoto mwenzake kisha kukamatwa na
kunusurika kuuawa na wananchi wenye hasira zaidi ya 300.
Raia wenye hasira kali wakimsubiri kwa hamu mtoto huyo nje ya nyumba aliyohifadhiwa.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,
Mama Seleman alisema: “Mtoto huyu alikamatwa kwa jirani yangu, Asha
Tembo akidaiwa kutaka kuiba mtoto wa mama huyo kwa njia za kichawi hivyo
mama huyo aliamua kupiga kelele na kumuitia mwizi.
Kamanda
akimbana mtoto huyo kwa maswali. “Mtoto alikuwa amevaa nguo nyeusi
ndipo umati ukajitokeza na kuanza kumshambulia kwa maneno makali huku
wengine wakimpiga vibaya na kutishia kumuua.
Makamanda wa Polisi wakimchukua mtoto huyo kwa usalama zaidi. “Baada
ya kuona watu wanazidi, nikaamua kumwokoa na kumficha ndani
kwangu.“Nikiwa ndani umati wa watu ulitishia kuchoma nyumba yangu lakini
nilifunga milango kisha nikawaita polisi wakaja kumuokoa mtoto huyo.”
Mtoto huyo akichukuliwa kwenye 'Defender' kuelekea kituo cha
Polisi.Kwa upande wake, mtoto huyo alisema: “Bibi ndiye huwa ananituma.
Kwa sasa niko kwenye ulimwengu wa giza na mateso makubwa.
Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Maria Vicent alisema: “Mwanangu
nilimzaa akiwa salama lakini tangu atoke Moshi (Kilimanjaro) kwa bibi
yake amekuwa wa ajabu hivyo nimepanga kumpeleka kwenye maombi.”
No comments:
Post a Comment