Marehemu akipakiwa kwenye gari tayari kumpeleka chumba cha kuhifadhia maiti.
Marehemu Gabriel Mwasyebule enzi za uhai wake.
Nyumba ya marehemu, Gabriel Mwasyebule anayotuhumiwa kuijenga kwa uchawi.
Moja
ya shamba la viazi vinavyo subiriwa kuvunwa mwezi huu, shamba la
marehemu, Gabriel Mwasyebule, mashamba amabayo pia ni moja ya sababu
ambazo wananchi wa lwangwa wanamtuhumu marehemu kuwa alikuwa
anawalimisha watu kiuchawi na kuiba mazao ya mashamba mengine kiuchawi
ili shamba lake liwe na mazao mengi na mazuri.
Hii ndio stoo kuwekea mazao mbalimbali ambayo marehemu alikuwa anatumia kutunzia mazao yake.
MATUKIO
ya kujichukulia sheria mikononi bado yanazidi kuyakumba baadhi ya
maeneo mkoani Mbeya ambapo katika tukio hili kijana Gabriel Mwasyebule
miaka 39 ameuawa na wananchi wenye hasira kali wakimtuhumu kwa imani za
kishirikina.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa kifo
hicho na kumtaja marehemu aliyetambulika kwa jina la Gabriel Mwandemwa
(Mwasyebule) mkazi wa kijiji cha Ikamambande (Lwangwa) Wilaya ya Rungwe
aliuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali
sehemu za kichwani na kifuani.
Alisema
tukio hilo lilitokea siku ya jumapili majira ya saa tano asubuhi huko
katika Kijiji cha Ikamambande, kata ya Lwangwa, Tarafa ya Busokelo,
Wilaya ya Rungwe, mkoaniMbeya
Alisema
taarifa za awali zinadaiwa kuwa, uongozi wa kimila kijijini hapo
uliitisha kikao cha dharura ukihusisha viongozi wa vitongoji na vijiji
jirani na ndipo waliamua kumtafuta na kumlazimisha marehemu kuhudhuria
katika kikao hicho na kisha kuanza kumpiga na kupelekea kifo chake.
Alisema
marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mshirikina kijijini hapo kwa kuwa
anawaroga watoto na kuwa anajipatia mazao mengi ya mavuno ya viazi na
kujipatia pesa zilizowezesha ujenzi wa nyumba yake aliyoweka marumaru na
Gipsam pia kumiliki pikipiki moja huku akitarajia baada ya mavuno
mazuri ya mwaka huu kununua gari la kutembelea.
No comments:
Post a Comment