Thursday, August 28, 2014

KIJANA APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA SIMU MBEYA



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Mwakilalo (25) mkazi wa Block T alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mbeya baada ya kupigwa na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa tuhuma za kuiba simu.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 02:15 usiku huko katika maeneo ya Block T, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa marehemu alikamatwa na kuanza kupigwa na wananchi hao na badae alipelekwa na kufungiwa katika ofisi za mtendaji ambapo alitoroka na ndipo wananchi hao walimuona na kumkimbiza na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kumvunja mkono wake wa kushoto na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya. Juhudi za kuwatafuta waliohusika katika tukio hilo zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wawafikishe watuhumiwa wanaowakamata kwa makosa/tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

No comments:

Post a Comment