Monday, August 25, 2014

KIJANA ACHOMWA MKUKI WAKIGOMBEA SHAMBA

MAPIGANO yakurushiana mishale,mawe na marungu yanayohusishwa na kugombea ardhi, yameibuka kati ya wananchi wa Kijiji cha  Sirorisimba wilaya ya Butiama na Kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda mkoani Mara na kusababisha baadhi ya wananchi kujeruhiwa kwa kuchomwa mishale na kukimbia makazi yao.


Tukio hilo limekuja kufuatia madai ya kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya hizo mbili huku ukimya wa viongozi wa wilaya ukitajwa kuwa chanzo cha kuibuka kwa mapigano hayo.


Wakiongea na Blog hii baadhi ya wananchi wa kijiji cha Sirorisimba  wilaya ya Butiama mkoani Mara wamesema mgogoro huo umeanza miaka mingi iliyopita ambapo wananchi kutoka kijiji cha Mikomariro wilaya ya Bunda wamekuwa wakivamia wananchi wa kijiji hicho lakini mpaka sasa hakuna hatua zinazochukuliwa na viongozi wa wilaya hiyo.

Walisema uvamizi wa maeneo makubwa uliofanywa hivi karibuni katika eneo hilo umesababisha mapigano makali na kusababisha mtu mmoja kuchomwa Mshale mgongoni na kulazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Mmoja wa majeruhi aliyechomwa mshale kwenye tukio hilo na kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara Hamisi Nyahanga amesema  alivamiwa kwenye eneo lake la kilimo na wananchi na kuambiwa siku zake za kuishi zimekwisha na kuamua kukimbia ndipo alipopigwa mshale wa mgongo .

No comments:

Post a Comment