Wanajeshi hao wa jeshi la nchi ya NEPAL wakiwa wanaonyesha vyeti vyao vya uanajeshi wa jeshi hili |
Idara
ya uhamiaji Jijini Dare s salaam imewakamata raia 12 wa kigeni waliokuja nchi
kinyume na sheria wakiwemo wanajeshi wanne wa jeshi la NEPAL pamoja na nane kutoka nchini
india walioletwa nchini kinyume na sheria kwa kisingizio cha maisha magumu
nchini kwao.
Raia hao wamekamatwa katika nyumba ya
kulala wageni ya ESCOT iliyoko kijitonyama jijini Dar es salaam katika
operation maalum iliyoendeshwa na idara ya uhamiaji Jijini baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo juu ya uwepo wa watu hao ambao
waliwatilia mashaka.
Afisa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO akizungumza na mtandao huu kuhusu sakata hilo |
Wanajeshi
hao wanne wa jeshi la NEPAL yumo pia komando mmoja wa jeshi hilo ambao nao
wamedai kuletwa nchini kwa ajili ya kutafutiwa ajira ya maswala ya ulinzi
katika nchi za Africa hivyo wakashukia Tanzania kama kituo kwa ajili ya
kufanikisha malengo yao.
Akizungumza na mtandao huu muda mfupi
uliopita afisa wa uhamiaji wa jiji la Dar es salaam GRACE HOKORORO amesema kuwa wahamiaji hao wamekuwa wakipita katika
nchi ya Tanzania na kupelekea nchi nyingine kama Africa ya kusini kwa ajili ya kufanyishwa kazi zisizo halali
Picha mbili zikionyesha wanajeshi hao wakiwa katika nchi yao wakiwa wanalitumikia jeshi la nchi yao kabla ya kutimka na kuja nchini |
Aidha amesema kuwa watu hao wamekuwa
wakiletwa na mawakala ambao wamekuwa wakiwatoa katika nchi zao kwa ahadi la kuwatafutia kazi katika nchi hizi jambo
ambalo amesema kuwa linatafsiriwa kama biashara ya binadamu ambapo mawakala
waliowaleta watu hao hadi sasa hawajapatikana.
Aidha
Bi GRACE amewataka watanzania na watu wasamaria wema kuwafichia watu
wanaowaficha watu kama hao kwani ni kinyume na sheria na baadae huleta madhara
makubwa kama uhalifu na uuzwaji wa madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment