UKATILI WA KUTISHAMAMA ADAIWA KUMSULUBU MTOTO, APEWA KIBANO
Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi
zilidai kwamba, Teddy alimchukuwa mtoto huyo jijini Arusha kwa lengo la
kumsaidia kukaa na mwanaye kwa kuwa familia ya mtoto huyo haina uwezo na
ameishia darasa la tatu kwa kukosa vifaa vya shule.
Kwa mujibu wa Teddy, bila kujua kwamba
ni kosa kumwajiri mtoto, aliamua kumwadhibu mtoto huyo kutokana na
kutomsikiliza bosi wake hasa alipokuwa akionywa kuachana na tabia ambayo
haikuwa ikimfurahisha.
Kwa upande wake Magdalena alidai kwamba
alikuwa akipokea kipigo kila siku hasa wakati mama huyo alipokuwa
akirejea nyumbani kutoka ‘jobu’ na kukuta mwanaye analia.
“Alikuwa akinipiga kila siku akikuta mtoto (wa miaka miwili) analia. Pia kuna siku alinipiga
sana asubuhi, nikaona nikimbilie kwa mjumbe, ndiyo tukaenda kituo cha
polisi, tukakutana naye akiwa anatoka polisi kutoa taarifa kuwa
nimepotea, mimi naomba nisaidiwe nirudi kwa mama yangu Arusha,” alisema
Magdalena na kumfanya bosi wake huyo apewe kibako na vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment