Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Wayahudi wanne wenye msimamo mkali wamekamatwa nchini Israeli baada ya kuzua rabsha katika sherehe ya kuadhimisha harusi ya mwanamke myahudi aliyebadili dini na kuwa Muislamu na kisha kuolewa na mwanamume Mwarabu rai ya wa Israeli. Mamia ya watu waliandamana nje ya ukumbi uliotumika kwa sherehe hiyo katika mji wa Rishon LeZion Jumapili wakipinga ndoa hiyo licha ya kuwepo kwa maafisa wa Usalama.
Bwana harusi , Mahmoud Mansour, alikuwa amechukua hati ya mahakama ya kupinga kufanyika kwa maandamano ya kupinga nikaha yake lakini maafisa wa usalama wakashindwa kuzima maandamano hayo
Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Bi Harusi Morel Malka, alikuwa amewaalika wageni 500 katika hafla hiyo.
Bi Malka, 23, alikuwa amesilimu kabla ya sherehe hiyo kuambatana na desturi za kiislamu.
"Kwa kweli tunaishi pamoja kwa amani na sielewi kwanini ndoa hii inawahusu watu." alisema bwana Mansour, 26.
Rais Rivlin alifananisha maandamano hayo dhidi ya ndo hiyo na ''panya anayengata msingi wa unaoliunganisha taifa hilo la Israeli''.
Maandamano kupinga ndoa kati ya Myahudi na Muarabu nchini Israel
Rais wa Israeli Reuven Rivlin amekashifu upinzani dhidi ya ndoa hiyo .
Muungano wa wayahudi wenye msimamo mkali Jewish Lehava walipewa ruhusa ya kuandamana kupinga ndoa hiyo ilimradi tu wasikaribie chini ya mita 200 karibu na ukumbi wa sherehe hiyo.
Kundi hilo linapinga ndoa kati ya Wayahudi na Waarabu.
Waandamanaji wanne walikamatwa na polisi kwa kukiuka masharti yao kulingana na mtandao wa habari wa kiyahudi.
Sadfa ni kuwa kundi lingine linalounga mkono ndoa kati ya Waarabu na Wayahudi lilifanya maandamano kuunga mkono ndoa hiyo na hivyo kuwalazimu maafisa wa usalama kufanya kazi ya ziada kuzuia makabiliano baina ya makundi hayo hasimu.
No comments:
Post a Comment