WATU wenye hasira wamempiga hadi kumuua mwanamume, aliyemuua mke wake kwa kumpiga rungu tumboni.
Kamanda wa Polisi
mkoani hapa, David Misime, alisema tukio hilo la Septemba 20, mwaka huu
katika Kijiji cha Mzogole wilayani Mpwapwa, ambapo mtu mmoja, Mwajuma
Chomola (48) aliuawa kwa kupigwa na rungu tumboni upande wa kushoto na
mume wake, Richard Kodi (55).
Hata hivyo, alisema Kodi naye
aliuawa Septemba 21, mwaka huu baada ya kushambuliwa na wananchi
waliojichukulia sheria mkononi. Alifariki dunia akiwa anaendelea na
matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.
Aliuawa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo, amekufa baada ya kupigwa na mtu huyo.
Misime alisema uchunguzi wa awali, unaonesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi.
Kamanda
huyo alisema Kodi alimuua mkewe huyo, aliyekuwa akiishi naye baada ya
kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe, iliyokuwa kijijini hapo,
akidhani kuwa alikuwa ameenda kwenye masuala mengine.
No comments:
Post a Comment