Mshtuko!
Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas
Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri
wake, Ijumaa limesheheni data.
Mara
baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai
kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii
mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji
uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh!
Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la
kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina
lake lichorwe gazetini.
Kwa mfumo
wa elimu nchini ulivyo, mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na kati ya
miaka mitano hadi saba, jambo ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani
hesabu zinakataa hata kwa mtu asiyesomea mahesabu.
Ukiachilia
mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua kati ya miaka miwili
hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya elimu ya msingi (primary), miaka
minne ya sekondari (ordinary level), miaka miwili ya kidato cha tano na
sita (advanced level) na miaka mitatu ya shahada kwanza (bachelor
degree), jumla ni miaka 16.
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA MIWILI?
Kwa
mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi atakuwa
alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo ni msamiati
mpya kwa jamii ya Kibongo.
Ili
kuondoa utata na tafrani inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hadi
kufikia hatua ya watu kutukanana, gazeti hili lilimtafuta baba mzazi wa
Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, Dar kwa leseni ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu alipopatikana alifunguka:
“Umri
wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile (miaka 18), kama mnataka
kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania mtaoneshwa passport (hati
ya kusafiria) yake…,” alisema mzazi huyo huku akiomba aachwe kwanza
ashughulikie wananchi wa jimboni kwake.
Hata kama
tukiamini maelezo ya mzazi, maana yake ni kwamba mrembo huyo alianza
darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo linazidi kuongeza
utata katika sakata hilo.
AKATAA KUHITIMU MASTERS
Alipobanwa
zaidi kuhusu taarifa zinazosema kuwa mwanaye amehitimu masters, mzazi
huyo alikanusha na kudai kwamba mwanaye amehitimu bachelor
degree(shahada).
“Kuhusu
masters mnakosea, mwanangu hana masters, ana bachelor, nilimshauri
achukue masters lakini akaomba nimuache ashiriki kwanza mashindano ya
u-miss ndiyo aje aendelee baadaye,” alisema mheshimiwa huyo.
NI AIBU NYINGINE KWA LUNDENGA?
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, suala la warembo kudanganya umri
limekuwa ni sugu hivyo kuleta tafsiri ya aibu kwa muandaaji wa
mshindano hayo, Hashim Lundenga akidaiwa kupigwa changa la macho pindi
anapowapokea katika mchakato wa awali.
Alipotafutwa Lundenga ili kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“I can’t answer that question (Siwezi kujibu swali hilo)…siwezi.”
SITTI ANASTAHILI KUWA NA UMRI GANI?
Ukiachilia
mbali muonekano, baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema
kuwa ukifuata utaratibu wa mfumo wa elimu Bongo, Sitti alipaswa angalau
awe na umri wa miaka 23, hata kama madai ya kurushwa madarasa ni sahihi.
No comments:
Post a Comment