BABU WA MIAKA 62 AMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA MITANO,,HEBU ANGALIA ILIVYOKUWA TU
Mzee wa miaka 62, Rashid Mbogo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka mitano.
Mtuhumiwa
huyo, mkazi wa Kijiji cha Vikonge kilicho katika Kata ya Mpandandogo
wilayani Mpanda, alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Chiganga
Ntengwa na kusomewa mashtaka na mwendesha mashtaka ambaye ni mkaguzi
msaidizi wa polisi, Naathaniel Silomba.
Ilidaiwa na mwendesha mashtaka huyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 19, mwaka huu saa 2:00 usiku akiwa nyumbani kwake.
Mwendesha
mashtaka huyo alidai kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa akiwa anasubiria
chakula cha usiku wakati kikiandaliwa na mkewe, alimwita mjukuu huyo na
kisha kumpakata mapajani. Alidai kuwa baadaye alivua nguo na kuanza
kumbaka huku mtoto huyo akipiga kelele za kuomba msaada kwa kitendo cha
babu yake.
Mwendesha
mashtaka huyo alidai kuwa baada ya kusikia mayowe hayo, bibi wa mtoto
huyo na majirani waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mtoto sebuleni
akiwa anatokwa na damu nyingi sehemu zake za siri huku analia kutokana
na maumivu makali aliyokuwa ameyapata.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo ambayo alikuwa amesomewa na mwendesha mashtaka.
Hakimu Chiganga aliieleza mahakama kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi endapo mshtakiwa atatimiza masharti.
Mshtakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo alipelekwa rumande.
No comments:
Post a Comment