Mike
Sonko ni yule Mwanasiasa mwenye vituko ambae alipata umaarufu sana toka
akiwa mbunge kwa kuwa na swagg zake kivyakevyake, alikua mbunge kijana
ambae anaingia na hereni bungeni, blingbling kibao kama cheni na pete
kama anavyoonekana ametupia kwenye hii picha hapa juu akiwa sasa ni
Seneta wa jiji la Nairobi.Sasa juzi kati Rais Uhuru Kenyatta alikwenda
The Hague Uholanzi kwenye Mahakama ya ICC kwa hiyo Wakenya wenzake
wanaopinga huo uamuzi wa ICC na kuona ni usumbufu wakajilipia nauli zao
ili kwenda kumsupport ambapo Seneta huyu ni mmoja wa waliojilipia na
kulipia wengine pia.
Pamoja na
Sonko kwenda huko akiwa na dukuduku la kukerwa na maamuzi ya Mahakama
hiyo akiitaka imuache Rais wao wa Kenya afanye kazi, aliamua kuvaa
tshirt yenye maandishi ya Kiswahili ‘ikiwatusi’ Wazungu kama
anavyoonekana kwenye hii picha hapa chini.
Kwenye
hizi picha hapa chini anaonekana Seneta wa jiji la Nairobi Mike Sonko
akiwa amewasili mahakamani ICC na kikosi chake kisha wakafanya
maandamano mafupi kabla ya kumpa support Rais Uhuru kwa kuimba wimbo wa
taifa na nyimbo za kizalendo wakati kesi ya Uhuru ikiwa inaendelea
Mahakani.
Tayari
Rais Uhuru Kenyatta amerejea Kenya jana asubuhi na kupokewa na maelfu
ya Wakenya ambao hawakupendezwa na kilichofanywa na Mahakama hiyo.
Muda
mfupi tu baada ya kuwasili jana Rais Kenyatta alipiga vijembe Mahakama
hiyo kwa kusema ‘Walikua wanafikiria kwamba tutakataa kwenda mi
nikawaambiwa ile kitu itakataa kuja huko ni Urais wa Wakenya, tumeenda
tumekaa huko masaa matatu hatujaambiwa chochote… hatukufungua mdomo sasa
hata nashindwa kujua nilikwenda kufanya nini’
‘Ile kitu
hawajafahamu kwa vichwa vyao ni kwamba kama nchi ya Kenya tumetoka
safari ndefu, na wasifikiri ya kwamba hatujui ni mahali gani tulifanya
makosa, sisi tunawaambia hapana….. tuko na suluhu ya shida zetu’
No comments:
Post a Comment