Na Father Kidevu Blog.
Bomba
la mafuta linalotumika kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Dar es
Salaam Tanzania hadi Nchini Zambia lijulikanalo kama TAZAMA limetobolewa
na mafundi waKampuni ya Raddy Fiber Solution Ltd ya jijini Dar es
Salaam wakati wakichimba chini ya barabara kupitisha awamu ya pili ya
kebo za mkongo wa taifa wa mawasiliano katika eneo la Gongo la Mboto
jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni ya Raddy, Rajab Mikumwo amesema
mafundi wake walitoboa bomba hilo kwa bahati mbaya majira ya saa nane
alasiri leo wakati wakifanya kazi ya kuchimba njia ya kupitisha bomba.
Sehemu inayoonesha mafuta ya kimiminika baada ya bomba hilo kutobolewa chini. Wakazi wa Gongo la mboto wake kwa waume wakiwa katika pilika za kuchota mafuta hayo machafu ya Diseli.
Mkazi wa Goms akiondoka na dumu lake la mafuta.
Mafuta hayo yakitiririka katika mtaroni mithili ya maji.Picha Kwa Hisani ya Father Kidevu Blog
No comments:
Post a Comment