Baadhi ya watu wakiwemo watoto wakiangalia mwili wa kijana aliyeuawa kwa
kupigwa na baadaye kuchomwa moto eneo la kata ya Kiloleni manispaa ya
Tabora ambapo kwa taarifa kutoka kwa vyanzo vyetu zimeeleza kuwa kijana
huyo alitekwa na kundi la vijana wenzake majira ya usiku wakigombea
msichana hatua ambayo ilisababisha kufanyiwa unyama huo uliosababisha
kifo chake.Hata licha zogo kubwa lililotokea lakini hakuna mwananchi
hata mmoja aliyejitokeza kwenda kumsaidia kijana huyo ambaye hadi umauti
unamkuta hakuna mtu aliyemfahamu mara moja huku vijana waliotekeleza
unyama huo wakitokomea kusikojulikana.
CHANZO:KAPIPIJ BLOG
No comments:
Post a Comment