Tajiri
maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari. Tukio
hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18, mwaka
huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia, kabla ya
kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST lenye namba
za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na kimada wake aliyetajwa kwa
jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini Bukoba.
KIFO
cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho
kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya
marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo
hadharani juu ya kila kitu kilichotokea
Mwili
wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Bukoba
kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa siku ya leo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki
Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa pombe kali aina ya Whisky Bond pasipo
kula vizuri huku akisumbuliwa na tatizo la presha hivyo wakati akifanya
yake ndani ya gari, ghafla presha ilipanda, akaanza kutapatapa.
“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo na anasumbuliwa na presha,
sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa ndiyo kilitibua zaidi. Pombe
ukiwa hujala huku una tatizo la presha madhara yake ndiyo haya,” kilisema
chanzo chetu.
Baada ya hali yake kubadilika ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake
badala ya kukimbia kama ambavyo wengine hufanya, yeye alifanya juhudi
kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa kupiga simu kwa marafiki wa marehemu,
lakini kabla hawajafika, mtu mmoja alitokea na kumsaidia marehemu
kumpeleka katika kituo cha Afya cha CLCT-Ndolage.
Chanzo hicho kilizidi kusema kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea
kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki
kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda
mbio sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya marafiki wa marehemu waliingiwa hofu
na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi wakihoji chinichini kwamba pengine
alimpa marehemu kitu kibaya.
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo,
walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye
madhara,” kilisema chanzo chetu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea
kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya
upelelezi zaidi.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu
maeneo ya Kyakairabwa, kata ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona
aibu kuzungumzia kifo chake hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa
marehemu alikuwa mtu anayeheshimika katika jamii.
Jeneza
la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu, bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo hicho.
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na
kifo chake, daktari mmoja mtaalamu wa
magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha
mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.
“Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine
wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu
inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano
wa kupoteza maisha ni mkubwa.
“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya
presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali
kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya
vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
Mfano
wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,” alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana mjini humo.
No comments:
Post a Comment