Sunday, June 16, 2013

MLIPUKO WATOKEA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA, BOMU LAJERUHI NA KUUA JIJINI ARUSHA







 




Majeruhi. Mungu urehemu tz
ARUSHA.
MKUTANO wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa.
Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhur iwa na mamia ya wananchi.
Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11.
Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo.
Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia.
Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki.
Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani.
Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo.
Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki.
Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo. CHANZO MWANANCHI.

Sunday, June 9, 2013

WAANDISHI WA HABARI WAPATA NAFASI YA KUWATEMBELEA WADAU WA KILIMO MKOANI ARUSHA CHINI YA B4FA TANZANIA






 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari  Tanzania bara na Zanzibar walipata fursa ya kutembelea wadau mbalimbali wa kilimo wakiwemo wakulima wenyewe ili kujionea hali halisi katika sekta hii nchini. Waandishi hao ambao walipata fursa hiyo chini ya bioscience for farming in Africa nchini ( B4FA) walitembelea wakulima, watafiti wa mbegu, tissue cultures pamoja na wakaguzi wa mimea nchini. Fursa hiyo ilitolewa ili kuruhusu waandishi wa habari kujionea uhalisia wa mambo na kujipanga upya kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora kinachoendana na zama hizi za digital katika kutumia sayansi na teknolojia ili kujikwamua kiuchumi. Kama ijulikanavyo kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania bado sekta hii imeachwa nyuma na msemo huo kubaki vitabuni na si kiuhalisia. pamoja na jitihada za serikali kujikita katika kilimo kwanza pia zana hii imebaki kuwa maneno na si kimatendo kwakuwa mkulima wa Tanzania hajui nini manufaa ya kilimo kwanza.  Hata hivyo kilimo cha Tanzania bado kina changamoto nyingi ikiwemo kuwepo kwa mbolea feki, mbegu feki, ukame, pamoja na ushirika mdogo kati ya wataalam na wakulima. Mambo ambayo inatakiwa kutilia mkazo kama kweli kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania ni kuanzia uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora kazi ambayo AVRDC ya mkoani Arusha wanaifanya.





Aina tofauti za mbegu zikiwa kwenye hatua za ukaushaji

Aina tofauti tofauti za mboga mboga zikiwa shambani


Baadhi ya Mbegu zikiwa zimehifadhiwa kiusalama kabisa katika chupa maalum kwa kazi hiyo AVRDC


Waandishi wa habari wakimuhoji Bwana Hassan Mndiga kuhusiana na utaalam wake kuhusu mbegu wanazozalisha.


kilimo bila kushirikiana na wataalamu ni kazi bure kwani ni sawa na kipofu kumwongoza kipofu mwenzie. msemo huu naniufananisha na jinsi ambavyo wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao bila kupata mwongozo kutoka kwa wataalam. Ili mkulima aweze kufanikiwa nilazima mbegu anazozitumia ziwe bora, mvua za kutosha pamoja na kufuata kanuni zote za kilimo. AVRDC ni wazalishaji na watafiti wa mbegu mbalimbali kwa ajili ya matumizi kwa wakulima. kiwanda hiki kimekuwa mstali wa mbele kufanya utafiti wa mbegu bora kulingana na mazingira husika. Lakini imekuwa ni kazi ngumu kwa mbegu hizi kuwafikia wakulima kutokana kwamba wao huzalisha na kufanya utafiti na kuwapa wauzaji ili kuzifikisha kwa wakulima, lakini kwa bahati mbaya sana wakulima huzipata mbegu hizi kwa kuchelewa na wakati mwingine hupata mbegu feki kutokana nachangamoto mbali mbali zilizopo katika sekta ya kilimo. Serikali yatakiwa kujipanga ili kumwinua mkulima kwani mara zote tumekuwa tukisema kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa Tanzania lakini  bado sekta hii imeachwa nyuma. Viwanda kama AVDRC vipo nchini mwetu lakini ni wakulima wachache sana wanaojua uwepo wa viwanda hivi na wakati  mwingine watu hutumia nembo yao kuuzia mbegu feki kwa wakulima wakati wao si wauzaji bali ni wazalishaji na watafiti. AVDRC  wamekuwa mstari wa mbele kuzalisha mbegu zinazostahimili hali ya hewa ya mahali husika.


Imekuwa ni dhana ya watu wengi kuona kilimo hakina manufaa baada ya kuona nguvu nyingi hutumika katika kilimo lakini mafanikio ni madogo tena yasio na tija kwa wakulima na kubaki akiwa ndio wenye kipato duni nchini. Dhana hiyo ambayo Bwana Allan anaiona ni kinyume mara baada ya yeye kugundua siri ya kufanya kazi ya kilimo kwa kufuata ushauri kutoka kwa wataalam. Allan ambaye ni Mmeru, mkulima na mkazi wa tengeru wilayani Meru Mkoani arusha amekuwa mfano wa kuigwa kwa majirani na marafiki kwakuwa yeye amepata manufaa makubwa kupitia kilimo. kitu ambacho kimemsaidia kubadili maisha yake kiujumla kwani amekuwa akilima mara tatu kwa msimu kwa kutumia begu zilizoboreshwa (hybrid) na kulima kwa kubadili mazao shambani {crop rotation}ili kuepusha mazao kushambuliwa na magonjwa kitu ambacho anadai kutokukifanya hapo awali kabla hajakutana na wataalamu wa kilimo kwa ushauri. Pia bwana Allana ameomba wataalamu wa kilimo kufanya kazi bega kwa bega na wakulima kwani uwezekano wa kubadili hali ya mkulima wa chini kutoka katika hali duni na kufika juu zaidi inawezekana endapo kama watakuwa ni wataalamu wa vitendo na si maneno kama wanasiasa.










Bwana Allan (wa kwanza kulia) akiwa na wenzake shambani kwake

Shamba la mahindi la Bwana Allan

Mbali na bwana Allani pia Bi Hellen George wa kijiji cha Hengorore, Kisongo Mkoani Arusha alitoa siri ya kubadili mfumo wa maisha yake kutika kwenye mkulima asiye na kitu mpaka kuwa mfano wa kuigwa kijijini kama sio na wanakikundi wenzake kutokana na kupata mafanikio makubwa kutokana na kufuata kanuni na hatua za kilimo bora. Pamoja na mji wa Kisongo kukumbwa na ukame kwa kipindi cha msimu wa kilimo kilichopita lakini Bi Helleni amefanikiwa kupata mavuno kutokana na kutumia mfumo wa kulima hahindi yakiwa yamechanganywa na mazao yakufunika udongo ili kuzuia upotevu wa maji toka ardhini(cover crop) mazao hayo ambayo ametumia kufunika udongo ni pamoja na ngwara, kunde pamoja na maharage. Mbinu hii ambayo aliipata kutoka kwa NGO's ya RECODA.


Bi Hellen akiwa shambani kwake na kiongozi wa B4FA

 
Mbegu za ngwara zao analolima Bi Hellen maalum kwa biashara

Shamba la migomba  ambayo ni moja ya matunda yanayompatia kipato Bi Hellen

Shamba la mahindi likiwa linamchanganyiko wa mazao mengine kama ngwara kunde kwa ajili ya kufunika udongo usipoteze maji kutokana na ukame


Wakulima wadogo wadogo kama Allana na Hellen ni mfano wa kuigwa na tutafika mbali kama elimu zaidi itatolewa kwa jamii nzima ili kukomboa nchi yetu kutoka kwenye janga la njaa. Kilimo kwanza isiwe ni mkakati wa kumkomboa mkulima kutoka kwenye kilimo cha jembe la mkono na kumpeleka kwenye trekta bali na mipango mingine ni lazima ifanyike. Ukame ndio huo umeshakuwa ni moja kati ya changamoto ambazo wakulima wanalia nazo lakini zipo njia mbadala ambazo zaweza kutumika ili mkulima aendelee na kilimo chenye manufaa. Mbali na hayo yote pia wapo wakulima waliojidhatiti katikakuzalisha mbegu zisizo na magonjwa kwa kutumia tussue kama afanyavyo Bwana Mushobozi wa Kisongo Arusha. Yeye huzalisha mbegu za migomba, mihogo, pamoja a mahindi ambapo Serikali ni lazima ichukuwe mkondo wake katika kuwasaidia watanzania waliojitolea kwa hali na mali katika kuwainua wakulima wadogo wadogo

mbegu za migomba zikiwa katika hatua ya awaali


Watanzania inabidi tuondokane na mtazamo duni wa kuongea na kupanga sana bila kuwa na utekelezaji kitu ambavyo ni ugonjwa mkubwa nchini. Msemo huu unakuja kutoka na kwamba wataalamu wengi wapo sana maofisini wakitoa maagizo bila ya kuwa mstali wa mbele katika utekelezaji. Viongozi wa serikali inabidi kuondokana na mtazamo wa kimazoea na kubadirika ili kufanya kazi zenye tija kwa jamii haswa katika sekta  muhimu kama kilimo. Wapo mawaziri ambao hawajawahi hata siku moja kuwatembelea wakulima na kuwauliza matatizo yao kitu ambacho hakifai kabisa kutokea. Viwanda kama TBL badala ya kudhamini burudani na mpira isisahau kuwa ngano na shairi ni mazao wanayoyatumia kuzalishia vinywaji hivyo ni wajibu wao pia kudhamini tafiti za begu bora za mazao haya ili kuepukana na ghalama za kununua mazao hayo kutoka nje na badala yake wakulima wa ndani watalima na kuwanufaisha wao pia.
Mwandishi wa TBC Taifa Greyson Mutembei akimuhoji mtafiti wa gano na shairi Bwana Mamuya.

 Hata hivyo waandishi wa habari hawakusita kutafuta undani wa habari kuhusu uwepo wa mbegu za GMO kitu kilichowafanya kwenda TPRI na kukutana na mkaguzi wa mimea chini ya wizara ya kilimo Bwana Oshingi Shilla ambaye aliwahakikishia kuwa mpaka sasa hakuna mbegu ya aina yoyote nchini ambayo ni ya GMO. Hata hivyo alisema kuwa GMO si kwa kila zao au kila mbegu bali kuna mazao ambayo ni sumbufu hayo ndiyo ambayo yatafanyiwa utafiti kuyaweka katika mfumo wa vinasaba na watafanya hivyo endapo watagundua kuwa mbegu hizo zitakuwa na manufaa kwa wakulima wenyewe pamoja na watumiaji kwa ujumla.

Bwana Oshingi Shilla (wa pili toka kushoto) akiongea na waandishi TPRI

Waandishi wa habari wkifuatilia kwa makini maelezo ya Bwana Oshingi Shilla