MSICHANA mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka),
amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri
yake na kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa
kuwa ni wivu wa kimapenzi.Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa
Singida, wodi namba mbili ya wanawake, Anna Sprian ameifahamishakuwa
binti huyo amejeruhiwa sehemu za sikio la upande wa kulia na mgongoni,
ambapo amesema hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri kutokana na
matibabu anayoyapata hospitalini hapo.
Akizungumza Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa jina la Pendo, amesema majeraha ya moto katika sehemu ya sikio la upande wa kulia na mgongoni.
Majeruhi,
Jackline Lasway, akiwa amelazwa katika wodi ya wanawake katika
Hospitali ya mkoa wa Singida, baada ya kujeruhiwa kwa kumwagiwa uji wa
moto wakati akiwa dukani kwa bosi wake katika Manispaa ya Singida
Pendo
amesema kuwa tukio hilo limetokea jana Jumamosi Agosti 9, 2014 saa nane
mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la,
Charles Kamnde.
Amesema
akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo,
gafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na kuwa
alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka kujiokoa ili
usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la kulia na
mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa kisu
kutaka kumchoma kifuani.
“Mimi
sikuwa na ugomvi naye wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na
kunifanyia vile jana, maana kama ni kazi mimi ninafanya kulingana na
maelekezo kutoka kwa bosi wangu Chale lakini sijui kilichomfanya
afikirie kunifanyia huu unyama” alisema.
Aidha,
amesema katika purukushani za kujiokoa kuwa asichomwe kisu hicho,
alifanikiwa kumkamata mkono mwanamke huyo na kupiga kelele za kuomba
msaada ambapo watu walifika na kumwokoa baada ya muda mchache ambapo
alichukuliwa na bosi wake hadi Kituo cha Polisi mjini Singida na kupewa
PF3 kwa ajili ya matibabu na kupelekwa katika hospitali hiyo ambako
amelazwa huku akiwa ma majeraha mwilini.
Kwa
upande wake, mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani maelezo
aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti na baadhi ya majirani wa familia hiyo, wameonyesha
masikitiko yao juu ya tukio hilo na hatua ya mwananmke huyo kummwagia
uji msichana huyo huku wakihusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi baina
ya mfanyakazi huyo na mume wa mtuhumiwa.
“Kama
aliona kama kuna sehemu kamkosea angemuonya au kama ameshindwa
kueleweka basi angemshitaki hata polisi kwani kitu alichokifanya
hakiendani na haki za binadamu kwakuwa ni kumdhalilisha huyu msichana
ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato chake na
familia yake.
Kamanda
wa Polisi Mkoani hapa, Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuwa wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na mara baada ya
upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo
No comments:
Post a Comment