MJUMBE WA UKAWA AWASALITI WENZIE KWA KWENDA BUNGENI DODOMA
Dodoma. Wakati wajumbe wa Bunge la
Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na
msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja
wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa
6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo
Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi)
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa,
pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama
hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia
wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki
vikao vya Bunge hilo.
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni
No comments:
Post a Comment