Monday, August 11, 2014

MAKAMANDA WA MATAWI WA UMOJA WA VIJANA WA CCM KATA YA KIMANGA WALIVYOSIMIKWA

Dotto Mwaibale
VIJANA nchini wametakiwa kuwa makini kwa kutumiwa na wanasiasa ili kuvuruga amani na usalama wa nchi uliodumu kwa muda mrefu.

Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM), Khamis Juma Sadifa wakati wa hafla ya kuwasimika makamanda tisa wa umoja huo wa matawi katika Kata ya Kimanga jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

"Ninyi vijana ndio walengwa wakubwa kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani na usalama wa nchi hivyo kuweni makini katika jambo hilo kwani tunachokihitaji ni amani na usalama wa nchi kwa watu wote na itikadi za vyama vyetu" alisema Sadifa

Sadifa alisema hata nchi hii ikitokea kuongozwa na chama kingine lakini bila ya kuwa na amani ni kazi bure hivyo ni vema kila mmoja wetu akatambua kuwa hana budi kuilinda amani iliyopo na usalama wa nchi.

Katika hatua nyingine Sadifa alitoa baraka zake kwa Kamanda wa Vijana wa CCM wa Kata ya Kimanga iliyopo Wilaya ya Ilala, Scollastica Kevela kuendelea na utendaji kazi wake wa kuinua uhai wa chama katika kata yake kwa kuwatembea vijana na wanachama ili kujua changamoto zinazo wakabili.

"Nakuomba kamanda wangu Kevela endelea kufanya kazi yako ni kuimarisha chama katika matawi kwa kukukutana na vijana na si kukiuka sheria ya kuanza kufanya kampeni kama inavyodaiwa" Sadifa alitoa onyo.

Sadifa aliongeza kuwa kazi kubwa ya ukamanda wa vijana ni kuwakutanisha vijana na kusikia changamoto walizonazo na kuziwakilisha ngaji ya juu kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.

Kwa upande wake Kevela alisema kazi ya kuwainua vijana kiuchumi ndio kipaumbele chake cha kwanza na atahakikisha anafanya hivyo kupitia vikoba ambako yeye ni Makamu wa Rais wa chama hicho nchini.

Alisema amekuwa akifanya ziara katika matawi mbalimbali kwenye kata yake ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake ya kuimarisha chama hangamoto zinazowakabili vijana hao.


Katika hafla hiyo Sadifa alitoa vifaa vya michezo jezi na mipira kwa vilabu mbalimbali vya matawi katika kata hiyo ikiwa ni pamoja na fedha za ujenzi wa ofisi ya CCM katika eneo hilo ambapo zaidi ya sh. 500,000 zilipatikana.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa, akielekea meza kuu tayari kwa shughuli ya kusimika makamanda hao.
Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kata ya Kimanga, Scollastica Kevela (katikati), akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kusimikwa kwa makamanda tisa wa vijana wa matawi katika Kata ya Kimanga Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Khamis Juma Sadifa na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Ilala, Alfred Tukiko.Wanachama tisa wa Matawi Kata ya Kimanga wakila kiapo baada ya kusimikwa.

No comments:

Post a Comment