Nabii Samwel Mahela wa Kanisa
la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikocheni A (katikati
mwenye suti), akitoa huduma ya maombezi katika kanisa hilo.
MSANII wa Filamu aliyejitambulisha kwa
jina moja la Jane amedai amepona ukimwi baada ya kuombewa katika Kanisa
la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikochezi A.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanila hilo Dar es Salaam mwanzoni mwa
wiki hii wakati akitoa ushuhuda wa kupona ugonjwa huo alisema ana
mshukuru mwenyezi mungu na Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Nabii
Samweli Mahela kwa kumuombea na kupona.
"Nampashukurani zangu mungu kwa kuniponya kupitia mtumishi wake Nabii
Mahela nimeteseka sana na ugonjwa huu aleluya sasa nimepona"alisema Jane
na kushangiliwa na waumini wa kanisa hilo.
Jane alisema alianza kuugua ugonjwa huu zaidi ya miaka 10 iliyopita na
kupata matibabu katika hospitali mbalimbali bila kupata nafuu mpaka
alipoambiwa na mmoja wa waumini wa kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la
Onesmo kuwa kuna watu wanapona baada ya kuombewa katika kanisa hilo na
Nabii Mahela.
"Baada ya kuambiwa kuhusu uponyaji huo nilifika kanisani hapa na kuonana
na Nabii Mahela ambaye alinifanyia maombi mfululizo na kuona hali yangu
ikibadilika na sasa afya yangu imeimarika" alisema Jane.
Akizungumza kuhusu suala hilo Nabii Mahela alisema mbele za mungu
hakuna lisilo wezekana kama ilivyowezekana kwa Jane kwa kuwa aliamini
atapona kwa maombi na kweli amepata nafuu jambo la kumshukuru mungu.
"Biblia inasema kila aaminie atapona kwa jina la kristo na ndivyo ilivyotokea kwa Jane" alisema Nabii Mahela.
No comments:
Post a Comment