“Asiyefanya kazi na asile” hii ni
kauli ya Athumani Idd mfanya biashara wa matunda na mboga mboga Soweto jijini Mbeya.
Alitoa kauli hiyo alipotembelewa na mwandishi dukani kwake jijini Mbeya.
Athumani ni miongoni mwa wafanyabiashara wa
maaatunda ya tufaa, embe, zabibu na machungwa na kwa upande wa mboga mboga huuza
Uyoga, spinachi cornflower. Biashara hiyo aliibuni baada ya kutafuta ajira kwa
mda mrefu bila mafanikio hivyo alianza kujihusisha na kilimo cha mboga mboga na
kisha kuanza biashara hiyo aliyo nayo. Alisema “Vijana wengi wa mjini wamekuwa
wakilalamikia ugumu wa maisha kutokana na ukosefu wa ajira ambapo imepelekea
wengi wao kujihusisha katika vitendo vya uvunjifu wa sheria za nchi. Nimemaliza
chuo cha UDSM (University of Dar es salaam) nimesomea mambo ya biashara, lakini
sijabahatika kupata ajira hivyo nimeona nijiajiri mwenyewe kwenye kilimo cha
mbogamboga na uuzaji wa matunda kitu ambacho sijutii kukifanya na Napata faida
kubwa kuliko hata mshahara ambao ningelipwa. Na kati ya matunda yote niyauzayo
tufaa linauzika sana kuliko mengine yote.
Mbali na Athumani Idd pia wapo vijana
wengi sana ambao wamekuwa wakijishughulisha na biashara ya matunda hayo katika
sehemu mbalimbali za nchi yetu haswa mijini. Hapo awali lilionekana ni tuda
linaloliwa na watu wenye kipato kikubwa au watu wa mjini peke yao kitu ambaocho
kimekuwa tofauti kwa sasa kutokana na uwingi wa matunda hayo na kuuzwa karibu
kila mahalli hata barabarani kitu ambacho hapo awali haikuwa hivyo kwani hapo
mwanzo tunda hili liliuzwa katika maduka makubwa pekee.
Mbali na biashara ya matunda ambayo
imeenea sana sehemu za mijini, tufaa ni Tunda pekee ambalo limeonekana kutoa
ajira kwa vijana wengi wanaojishughilisha na biashara hiyo. Na hiyo ni kutokana na tunda lenyewe kupendwa na watu
wengi pia upatikanaji wake hauna msimu maalum.
Kwa kuliongelea tunda hili ni tunda
moja maarufu duniani ambalo hupendwa kuliwa na watu wote bila kujali lika la
mtumiaji, hii inatokana na utamu, ulaini wake pamoja na faida za kiafya
zinazopatikana kwa kula matufaa. Na wakati mwingine limekuwa likitumiwa na
wapendanao ili kutoa ishara ya upendo baina yao
Matunda haya hustawi zaidi kwenye nyanda za
juu ambako joto sio kali, sehemu kama lushoto, mkoani Tanga, Arusha, miteremko
ya Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Njombe, Songea na sehamu nyingine nyingi zenye
hali ya hewa zinazofanana na hizo. Udongo unaofaa kwa kilimo cha tufaa ni wenye
rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji.
Unaweza
kupanda kwa kutumia mbegu au kwa kununua miche bora kutoka kwenye taasisiza
kilimo mfano Uyole Mbeya kwa wakulima wa nyanda za juu, Tengeru kwa wakazi wa
Arusha na SUA kwa wale wa Morogoro nk. kama utatumia mbegu basi ni bora kununua
mbegu bora au ukikosa mbegu basi jaribu kutumia zile utakazopata kutoka kwenye
tunda lenyewe kwa kufuata kanuni bora za kilimo
Kutokana na hilo ipo haja ya
serikali ya nchi yetu kuona kwamba hiyo ni fursa tosha kwa wakulima kupewa
mafunzo na kuwawezesha ili kujizatiti katika kilimo cha matunda pendwa kama
tufaa ili kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja kama si kwa taifa zima
Kwa sasa matufaa mengi yaonekanayo
barabarani huletwa Tanzania yakitokea Afrika ya kusini ambako ndiko mafanikio
makubwa yamepatikana kwa kilimo cha matunda barani Afrika. Na kilimo cha tufaa
nchini humo limefanikiwa baada ya utafiti wa mbegu bora (hybrid) kufanyika na
tufaa ni miongoni mwa tunda ambalo lilifanyiwa utafiti huo na ndipo mafanikio yalipopatikana.
Akiongea kuhusu kuruhusu kuingia kwa
matunda hayo meneja wa TFDA mkoani Mbeya Bwana Rodney Alananga, amesema kuwa
wao kama TFDA wamechunguza kwa umakini na wamehakikisha kuwa matunda haya
yanayotoka Afrika ya kusini hayana madhara kama ambavyo watu wengine wamekuwa
wakidhani na kuogopa kula matunda hayo kwa dhana ambayo wengi wao wamekuwa
wakisema yanamdhara kwa afya ya binadamu. “sisi kama TFDA huwa tunaruhusu
chakula kuingia nchini kama hakina madhara hivyo wafanyabiashara wanatakiwa
kufuata sheria za kibiashara mpakani kama vile kulipia ushuru na vinginevyo watu wayatumie tuu kwani
tunawahakikishia kuwa matufaa hayo hayana madhara ya aina yoyote” alisema
meneja Rodney
Kwa upande wa wakulima wao wameiomba
serikali kuchukua baadhi ya wakulima wanaotoka katika maeneo yanayolima matufaa
na kuwapeleka Afika ya kusini ili kujifunza kwa vitendo jinsi ya ukulima bora
wa matunda hayo ili wao pia waje kuwa mfano kwa wakulima wengine ili kuinua
kilimo cha matunda hayo Tanzania. “sisi mpaka leo tunalima matufaa yaleyale ya
zamani ambayo ukiyapeleka sokoni watu huyaita ya kienyeji na wengi hawayapendi kwakuwa yana radha ya
uchachu tofauti na yale ya kizungu” akimaanisha yale yatokayo Afrika kusini.
alisema Yuda Nyamirandu mkulima wa njombe
“Mkulima hashawishiki mpaka ameona
kwa macho ama sivyo utatumia nguvu kubwa sana kumshawishi mkulima kuwa mbegu
Fulani inafaida na ndio maana wakulima wa mahindi wanawekewa shamba darasa ili
waone na hii isiishie kwenye mahindi tuu” alisema Emmanuel Sanga
Akiongea kwa uchungu sana, Bwana
Emmanuel alisema anasikitishwa sana na serikali ya Tanzania ambavyo haijaweka
kipaumbele kujali kilimo kimatendo huku akitolea mfano jinsi wakulima ambavyo
wanapata shida katika miundo mbinu, pamoja na teknolojia duni katika kilimo. “
Ndio maana vijana wanaona hakuna haja ya kujitesa kuingia katika sekta ya
kilimo maana ni kazi ya mateso na ndio maana wanakimbilia mijini, lakini
serikali ingejali sekta hii hakuna kijana ambaye angekwenda mjini wote
tungebakia kwenye kilimo, lakini sasa matokeo yake hiyo kazi wanafanya wazee
wasiokuwa na nguvu matokeo yake njaa inaikumba nchi”
Ikiwa kama kuna uwezekano wa vijana
kupata elimu katika kilimo na kuwezeshwa kifedha ni hakika ya kwamba kilimo
kwanza ikatimia kuliko kuiacha kauli hii ikaendelea kubebwa na wazee peke yao
kama ilivyo sasa kwa vijana wengi kukimbilia mijini na kuwaacha wazee wakashughulika
na kilimo. Na malengo haya yanaweza timia ikiwa kila mtanzania atasumama katika
nafasi yake na kutimiza majukumu yake impasavyo.
Hata hivyo Tanzania bado hatujachelewa
kwani taasisi za utafiti zipo na hivyo utafiti ukifanyika Tanzania yaweza
kujikuta juu katika ramani ya wakulima bora duniani na kupata faida kubwa kama
wazipatazo wenzetu. Kwani mbegu bora ni chanzo cha tija na mapato kwa wakulima
na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment