Monday, October 13, 2014

BIBI NA BWANA HARUSI WANUSURIKA KIFO

bibi harusiBibi harusi Mariamu mduwa aliyenusurika kifo katika ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo akiwa naendelea na matibabu katika hospital ya  mkoa wa Kigoma

 
 
 
wawili hawa wamenusurika katika ajali ya mtumbwi iliyogharimu vifo vya watua zaidi ya 10 baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama ziwa Tanganyika
Akiongea na mtandao huu katika wodu namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
”Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo,kwakweli mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia mungu”alisema bibi harusi huyo
Muhanga mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
”Safari ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika kungekuwa na barabara tungepita barabrani”alisema Mhanga huyo
 


wahangaNdugu jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika kifo baada ya ajali ya mtumbwi kutokea katika kijiji cha kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma
bibi harusi
 
Naye muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa wamejuhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na mpaka sasa wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed alisema kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa,na miili sita kuopolewa pamoja na walionusurika 11,lakini bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi ambao bado haijapatikana kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya sabini.

 UOKOJIWaokoaji mbalimbali wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya mitumbwi iliyobeba harusi kutoka kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalya kutafuta miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana

No comments:

Post a Comment