MSANII nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kuingia mitini
na shilingi milioni moja alizolipwa kwa ajili ya kutumbuiza kwenye
uzinduzi wa albamu ya Injili ya John Lisu iitwayo Uko Hapa, Jumapili
iliyopita.
Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando.Kwa mujibu wa
chanzo makini, Rose alimegewa kiasi hicho cha pesa na Kampuni ya Msama
Promotion iliyoandaa uzinduzi huo uliofanyika ndani ya Ukumbi wa Diamond
Jubilee jijini Dar Jumapili iliyopita.
“Rose jamani ana mambo! Mnajua kama amemliza Msama (mkurugenzi wa
Msama Promotion) shilingi milioni moja? Alipewa ili atumbuize kwenye
uzinduzi wa albamu ya John Lisu lakini akaingia mitini.“Mbaya zaidi kila
alipopigiwa simu kuulizwa kwa nini hajafika Dar ile Jumamosi ili
Jumapili awepo ukumbini akawa hapokei simu.
Kikaendeela: “Rose ananishangaza sana, sikuwahi kufikiria kama anaweza kufanya hivyo, kikubwa
kinachowaumiza wengi ni kutopokea simu na ingekuwa vizuri kama angetoa
taarifa mapema kwa kutohudhuria kwake na sisi tungejua cha kufanya
mapema,” kilisema chanzo hicho ambacho kipo ndani ya waandaaji hao.
Chanzo hicho hakikuishia hapo, kiliendelea kuanika kuwa shutuma za
aina hiyo zimekuwa zikimuandama sana mwanamuziki huyo kiasi cha
kushindwa kuaminika na kudai kuwa hana njaa ya kutokomea na pesa hiyo
kwani ni kiasi kidogo sana kwake.
Msanii nyota wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando akizungumza
jambo.Risasi Mchanganyiko lilimsaka bosi wa Msama Promotion, Alex Msama
ambaye alikiri
Rose kutotokea kwenye uzinduzi huo licha ya kulipwa kiasi hicho cha
pesa na kilichomuumiza zaidi ni kutopokea simu za wasaidizi wake
waliotaka kujua nini kilimpata.
“Aliniangusha sana maana hata yeye nilimtangaza sana kwenye vyombo
vya habari kwamba atakuwepo, lakini matokeo yake ikawa kimya, sijui nini
kimempata lakini nitatoa tamko siku mbili hizi,” alisema Msama kwa
masikitiko makubwa.
Alipopigiwa simu Rose Muhando alikacha kuongelea suala hili
No comments:
Post a Comment