NYOTA wa kuigiza sauti za watu maarufu aliye pia mwigizaji wa sinema
za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ wikiendi iliyopita alijikuta
akiaibika kwa kuzomewa na kupopolewa kwa chupa za maji na mashabiki wa
Klabu ya Simba baada ya kuingia uwanjani na demu aliyevaa
‘kihasarahasara’.Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve
Nyerere’akiwa na mrembo huyo.Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20,
2014 ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya
Yanga na Mtibwa Sugar katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji
walishinda 2-0. Steve alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu
huyo mrefu kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano
na kijani (zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo
walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa
kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara
hadharani.
Mrembo huyo akikatiza mbembezoni mwa uwanja.Baadaye mwandishi wetu
alimfuta Steve na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema:
“Wale kunizomea ni haki yao ila mimi na mwenzangu tumeona kama
wametushangilia.”
Alipoulizwa uhusiano wake na demu huyo,Steve aligoma kujibu badala yake alikimbilia
kwa mwandishi mwingine na kuomba msaada. Mrembo huyo alipotakiwa
kuzungumzia tukio hilola kuzomewa na sababu za yeye kuvaa vile, alijibu
kwa mkato: “Kuzomea ni haki yao, mimi nawaona kama washamba tu.
No comments:
Post a Comment