NA
BARAKA LUSAJO, MBEYA
KIJANA mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Wajibu Astofu (16)
mkazi wa kijiji cha Lupata kata ya Ipoma katika Halmashauri ya Busokelo
wilayani Rungwe Mbeya amepoteza maisha baada ya kushindana kunywa pombe haramu
za viroba toka nchini Malawi zilizopigwa marufuku kuingizwa na kusambazwa
nchini.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mwenyekiti wa kijiji
hicho Pius Dibile alisema kuwa kijana huyo aliweka mashindano na mwenzake ya
kunywa pakiti kumi na moja pome hizo za viroba vyenye alcol 35 na kuwa
atakayemaliza angepata zawadi.
Alisema kijana huyo ndiye alikuwa wa kwanza kuanza
mashindano hayo na kufanikiwa kumaliza pakiti zote kumi na moja na ndipo
alipoanza kuishiwa nguvu na kujipigapiga na kupelekea serikali ya kijiji na
baadhi wa wanakijiji kufika eneo hilo na kufikia hatua ya kumkimbiza katika
hospitali ya misheni ya Itete iliyokaribu na eneo hilo.
Dibile alisema kuwa alipofika katika hospitali hiyo
madaktari wa zamu walijaribu kuokoa maisha yake kwa kumuwekea mashine ya
kumsaidia kupumua lakini hali ikazidi kuwa mbaya na hatimaye akakata roho na
kuwa viroba hivyo vilimkausha maji mwilini na kushindwa kupumua.
Aliongeza kuwa Serikali ya Kijiji hicho kiliitisha kikao cha
dharula na kutaka kumuajibisha aliyedhamini mashindano hayo kwa kununua pombe
hizo zilizopelekea umauti wa kijana Astofu na kuwa walikuwa wamechelewa kwa
kuwa alikimbilia kusikojulikana na jitihada za kumpata zinaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chripin Meela aliwataka wananchi
kutii agizo la Serikali na kwamba wao walipopiga marufuku waliona madhara ya
pombe hizo kwa watumiaji ambapo bado wafanyabiashara wasio waaminifu wanaingizo
pombe hizo na kuzisambazo kwa njia za panya na kusababisha maafa kwa wananchi.
Meela aliitaka serikali ya kijiji kumtafuta kijana huyo aliyedhamini
mashindano ya pombe hizo na kumkamata ili afunguliwe kesi ya mauaji ili sheria
ifuate mkondo wake na iwe fundisho kwa wengine na kuwa wananchi watoe
ushirikiano pindi wawaonapo wafanyabiashara hao wanaposafirisha biashara hizo.
No comments:
Post a Comment