Katika
hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda,
Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa
sebule yao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati
wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa
nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa
siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo
wake, Irene Steve (5).
Mama
mzazi wa Focus Saimoni (kushoto) akihuzunika kumpoteza
mwanaye.“Alipofika alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia
ndani, akanywa chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na
kumkuta tayari ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
Mama
mdogo wa Irene, Catherine Zakaria (kushoto) akiwa na mama mzazi wa
Focus Saimoni.“Nilimwambia Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi,
nilipomwangalia vizuri ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa
mama mdogo anayeishi jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria
alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia
mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila
mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema
wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya
komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.
Mdogo wa marehemu Focus Saimoni, Irene.
Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema
alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili
umeshushwa chini. “Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya
mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili
umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna
aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa
nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Marehemu
Focus Saimoni (9) enzi za uhai wake.’’Tukio hili lina shaka ndani yake,
mtoto wa miaka 9 anawezaje kujinyonga, kwa stress zipi? Kwa kweli
inasikitisha sana, jeshi la polisi lina wajibu wa kuchunguza ukweli wa
kifo cha mtoto huyo,” alisema mama huyo.Baadhi ya wananchi walioshuhudia
tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi
kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.
No comments:
Post a Comment