HALI bado tete! Polisi wa Kituo
cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina
moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira
kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere
iliyopo maeneo hayo.
Akizungumza na Uwazi lililofika
eneo la tukio ndani ya ‘dakika sifuri’, denti huyo aitwaye Laila alisema
licha ya kuitikia salamu ya jibaba huyo na kumuamkia bado aliendelea
kumchombeza na kila alipojaribu kumkwepa ilishindikana.
Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na
kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani ya gari lililokuwa karibu yake
ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya kuomba msaada na hatimaye
kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita njia.”
Mwanafunzi huyo aliendelea
kusema: “Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu
sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu hawajambo,
akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi nikakataa
kwa sababu mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu vingine kutoka
kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto kutekwa na Noah
nyeusi.
Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini
yeye akawa anaendelea kuniambia maneno yake na kuanza kunivuta ndipo
nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi nipige kelele ndiyo watu
wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga mpaka walipofika polisi.”
Gazeti hili lilizungumza na
mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na
tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya yote kwanza amuokoe na
kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba
kwanza mnilindie usalama wangu, hao jamaa wanataka kuniua bila sababu,
mimi wala sikuwa na nia mbaya na huyo binti wananizushia tu, nilikuwa
namsalimia tu,” alisema Omar kupitia upenyo mdogo wa juu ya dirisha la
gari alilohifadhiwa.
-GPL
No comments:
Post a Comment