Tuesday, October 21, 2014

POLISI WAMUUA MUHALIFU WA UGAIDI ARUSHA

Polisi mkoani Arusha yamuua kwa risasi mtuhumiwa Namba Moja wa milipuko ya mabomu katika mikusanyiko jijini humo na umwagiaji watu tindikali baada ya kujaribu kutoroka akiwa njiani kwenda kuonesha bomu alilokuwa amelificha maeneo ya Kondoa mkoani Dodoma.
  
KIongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary (Pichani)ameuawa na jeshi la polisi wakati  akijaribu kukimbia.
Inaelezwa kuwa
Yahaya Hassan ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wakati alipojaribu kutoroka akiwa chini ya ulinzi.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,SACP Liberatus Sabas (pichani) Alisema kuwa tukio hilo limetokea  Oktoba 19 mwaka huu majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati  akijaribu kuwakimbia polisi.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

"Mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyiwa mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa na jana alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia triki zake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo akapigwa risasi mbili"alisema Sabas.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuweza kuteketeza matukio ya uhalifu.

No comments:

Post a Comment